Hivi hii ya Msigwa kumlipua Mzee Ali Kibao ina ukweli gani?

Nakuulizeni nyie mnaodai msigwa kamchoma,wauaji hawakujua kuwa aliy ni strategist wa chadema mpaka msigwa amtaje?..na nini kimekuthibitishia kuwa kauawa kwa sababu za kisiasa?

Wewe unayejua tuambiae kauwawa kwa sababu gani .....!!?
 
Kwa hiyo ccm serekali na tiss yao wanaamini Mzee kibao ndo alikuwa strategist wa kupindua serekali

Huu uoga usio na uhalisia ni wa kijinga sana
Huoni jamaa alikua mwanajeshi, katumikia JWTZ huyo.

Ukiwa na power inabidi usiwe muoga, otherwise utaumiza wengi tu bure. Shida sisis huku wenye power ni waoga
 
Msigwa ataumiza wengi Sana kwa kutafuta cheo. Lkn Mungu yupo. Kama alihusika kumtaja Mzee wa watu damu yake itaangaika ktk maisha yake yaliyosalia.
 
F-uckoff
 
Niko hapa Kwamsisi wazee wamekubaliana kufanya yao zinatakiwa ndoo sita za mate kukamilisha hilo fataki linaloandaliwa lazima watu wafe vifo vya ajabu ajabu.
 
Moderator nilikuwa na made inayofanana na hii lakini mkaifuta😳
Moderators wa jf cjui ni robot au wanatumia Al?? , maana kwanza wako fasta kuliko kawaida na pili wanafuta hata vingine vya kawaida. bado sijapata jibu ila pia tuwape hongera Kwa kazi ya kulinda maudhui ya mtandaoni na kuondoka taarifa za uzushi
 
Kondoo alikuwa anapita akamuona simba akilia akiwa amenasa kwenye boksi la chuma(grili), simba akamsihi sana kondoo amuokoe na kumuahidi kuwa hatamuua wala kumla, lakini kondoo akakataa.... Baada ya simba kubembeleza sana na kwa upumbavu wa kondoo, akafungua lile boksi la chuma.

Sasa simba alikuwa na njaa kali mno baada ya kukaa kifungoni kwa siku kadhaa bila kula chakula... Mara moja alimrukia kondoo na kukaribia kumuua ili amle, lakini kondoo alimkumbusha kiapo chake.

Waliendelea kubishana hadi wanyama wengine waliokuwa wanapita wakauliza kulikoni? Basi simba na kondoo wote wakaelezea jinsi ilivyokuwa, lakini kwa hofu ya simba na kutaka kupata huruma machoni pa simba, wanyama wote wakamsapoti simba isipokuwa kobe ambaye alidai kuwa hakuelewa mazingira na stori yenyewe.

Sasa kobe akamuomba simba aoneshe mahali alipokuwa kabla ya kondoo kumuokoa, simba akamuonesha kobe kwa mguu wake wa mbele, pale... Kobe akamuuliza tena, "ulikuwa ndani ama nje kabla ya kondoo kuja??"...Simba akamjibu, "nilikuwa ndani".

Kobe akamuuliza tena simba, "sawa, embu ingia tena ili tuone jinsi ilivyokuwia vigumu kukaa ndani ya grili kwani sielewi stori hii yote vizuri"... Simba akaingia, na mara moja(chapu!), kobe akafunga lile boksi la chuma (grili)... Na simba sasa alikuwa amenasa tena!!

Kwa mshangao mkubwa, wale wanyama wengine wakamuuliza kobe "Kwanini?" na kobe akawajibu..."Kama tukimruhusu simba amle kondoo leo, bado atasikia njaa tena kesho na hatujui kati yetu ni nani atakayeliwa kesho..!!"

FUNDISHO

Usiunge mkono uovu leo kwa vile haukuathiri moja kwa moja, pengine kesho inaweza kuwa zamu yako.!!

Nafikri tunahitaji kobe wengi zaidi katika jamii yetu.
 
Inasikitisha sana,yuda iskarioti ameuza file la Late Meddy kwa wahuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…