Hivi hii ya mtoto wa kwanza kuwa makamu wa wazazi ni Tanzania pekee au kote?

Hivi hii ya mtoto wa kwanza kuwa makamu wa wazazi ni Tanzania pekee au kote?

Kina
Ndio kawaida huku, mara nyingine tunaonekana tunaringa kumbe watu tunaona majukumu yaliyopo yanatosha
Kinachouma hao ndugu wa pembezoni wakijipata hata kupitia wewe wanahangaikaga na familia zao sio wewe tena .
Ni bora usaidie nduguzo wa kuzaliwa nao hata wakikutupa haiumi sana maana unajua ulihangaikia damu yako hivyo mungu ni mwema watakukumbuka siku
 
Ukiacha kufanya majukumu ya mtoto wa kwanza kuna atakaye ichukua nafasi yako. Utagundua hilo wakati wa vikao vya familia.

Yule anayebeba majukumu ndiye anayesikilizwa, ndiye anayeheshimiwa, ndiye mwenye sauti pengine kuliko ya baba sema heshima hufata mkondo wake, ndiye anayeamua wawe na familia ya aina gani. Ndiye anayeamua identity na heshima ya familia kwenye jamii inayomzunguka.

Unaposikia familia ya Mengi au Familia ya Ongala, au Familia ya Kikwete, au Familia ya Osea, ile heshima ni matokeo ya kazi zilizofanywa na wazazi na uzao wao.
Kwani lazima kwenda kwenye hivo vikao vya familia?
 
Nilikuwa nasoma sehemu nikakuta kuwa watoto wa kwanza wanalalamikia kuwa "Makamu Mzazi". Yaani ni mtoto anayekabidhiwa jezi kabla mchezo hajauelewa. Mtoto wa kwanza anatarajiwa kulea wadogo zake na wazazi wake at the same time. Nadhani ukiona mtu amekomaa kimawazo, unauliza tu "Hivi wewe ni mtoto wa kwanza eekh"

Kwenye jamii ni ngumu kujua mtoto wa kati, ila wa kwanza na wa mwisho ni rahisi kumbaini. hivi hili suala la mtoto wa kwanza kuwa mzazi ni dunia nzima au ni bongo tu?

Mimi kwetu ni wa kwanza, aisee, naombeni mwenye kamba aniuzie kwa bei yeyote, nina kazi nayo
Haka ni kautaratibu ka watanzania tu bila shaka😂
 
Kwani lazima kwenda kwenye hivo vikao vya familia?
Hapana. Unaweza pia usiende. Mfumo wa maisha ni maamuzi binafsi. Ni wewe tu kupima, familia yako ina watu wa aina gani? Nisipojihusisha nao napoteza nini? Nina mbadala wa uwepo wao?
 
Ujue mtoto wa kwanza wazazi wanakuwa wageni wa suala la kuwa na watoto kwahiyo wanamjengea matarajio lukuki ya kutaka aje kuwa hivi au vile.

Vilevile wazazi wanakuwa bado wamoto wamoto, ni kama askari waliotoka tu deppo wakienda kutuliza ghasia sehemu usikae hapo kimbia mbio zako zooote vinginevyo wanakuua kama sio kukupa ulemavu
 
Na kama kuna mdogo wako mwenye kibunda cha kutosha hiyo nafasi ya "Makamu Mzazi" anaichukua kibabe. Ifike sehemu sisi wazazi wapya tuwalee watoto wetu kwa namna ya kuja kujisaidia wao na sio kutusaidia sisi. Hii kuzaa mtoto ili aje kuwa kitega uchumi baadae sio sawa. Wazazi wengi pia wanafanya kosa la ubaguzi kwa watoto wao kwasababu ya hali zao za kiuchumi.
 
Na tabia nyingine inayokera umeshakua mkubwa una maisha yako ila mzazi wako anakushikiria kutaka kukupangia kila kitu hasa wazee waliozaliwa kabla ya utawala wa Hayati Mwinyi.
 
Majukumu ni ngumu kuyaacha, ila nawaza namna ya kubadili utaratibu. Yaani mtoto wa kwanza unapewa majukumu mazito, wakati mwingine uko mtoto unaambiwe, "wewe ndio mkubwa", "Una wadogo zako" haya yote ni kukufanya uone tayari uko uwanjani.

Ukishaingia uwanjani ndio kimbembe kabisa, hadi mtoto wa shangazi unaletewa umuangalie wewe. Heshima unayopata ni ile tu "Huyu ndio atatuzika" yaani nazika mtu wakati mwenyewe sielewi dah
Ili ufanikiwe kwenye maisha jitoe ufaham tu. Potea miaka miwili hiv uone
 
B
Na tabia nyingine inayokera umeshakua mkubwa una maisha yako ila mzazi wako anakushikiria kutaka kukupangia kila kitu hasa wazee waliozaliwa kabla ya utawala wa Hayati Mwinyi.
Bro mbona mzee wa hivyo ni mbabu sana atakushauri nini huyo maana hata smart phone sidhani kama anaijua
 
Back
Top Bottom