Hivi hili ni ubinafsi uliopitiliza au tuitaje? Lipo sana kwa wachungaji na wanasiasa

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Wachungaji na wanasiasa kuomba waumini au wananchi wawachangie kununua vitu kama mfano magari au kuwachangia kufanikisha safari zao za kwenda Ziarani nje ambazo nyingine ni mapumzikoni tu .

Au kufanikisha mambo ambayo ni faida yake binafsi au mambo kama pesa ya Mwenge /ujenzi wa shule mambo ambayo Serikali inaweza gharamia

Unakuta walengwa ni watu ambao hata kula yao tu shida.

Tuitaje hili? Kibaya zaidi anachangiwa mtu mwenye uwezo mkubwa tu wa kifedha.​
 

Lissu amepigwa risasi 16 na nyingine 22 kuharibu gari kwa kuwatetea watanzania madini yao yasiuzwe.

Kipi kina thamani kati ya uhai na LC 300?
 
Bado huja sema in details wachungaji wa aina gani?

Na pila kama mada yako ilikuwa inamlenga mtu flani andika straight sio kuficha ficha tu
 
Cha kushangaza mkuu Hadi mwenge wa uhuru watu wanalazimishwa kuchangia.
 
tena unakuta anae omba achangiwe ana afya njema, akili timamu, ana uwezo na nguvu kabisa za kufanya kazi....

mi nadhani,
msingi wake ni malezi, mazoea na tabia mbaya wanazo endekeza baadhi ya wana siasa na hao wa huko kwa maombezi ambao ni wa binafsi sana na wanajiona wao ni special than special itself.

tabia hii isopokemewa kwa nguvu zote, hukomaa na kua ndio maisha ya mtu, kama ya ombaomba wengine huko mabarabarani. ni aibu na fedheha sana kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki au taasisi inayohusika
 
Mtu ana uwezo wa kununua gari ila hataki tumia pesa yake daaa
 
Tuliamua kama taifa siasa ndiyo iwe kazi inayolipa sana kuliko uweledi !baada ya hapo siasa ikaleta maisha magumu sana ndipo wajasiriamali was kiroho wakaona kukata tamaa wananchi ndio mlizamo wa kuwaunganisha Kwa Muumba kupitia matoleo !kwamba shida zao zitaisha!ndipo Hali ikawa mbaya zaidi Hadi sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…