Kwa sasa ukiwa na vijipesa kidogo na uthubutu basi unaweza vunja sheria yeyote ya nchi.
Anaepaswa kukemea hata hajui kinachoendelea as long as yake yanamnyookea. Yeye kauli yake moja tu, 'na hili mkalishughulikie'.
Kwa dalili zilizopo hizi taasisi zote za mikopo ya kausha damu zina baraka ya walioshika hatamu, hivyo hakuna chochote watachofanywa hao wanaovunja sheria.
Suluhisho ni dogo tu, usikope kwenye hizo taasisi kinyume na hapo kubali kuweka maisha yako rehani. Maana jamaa wakija kudai wana mpaka mamlaka ya kuua achilia mbali kuchukua samani zako.