Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Uza kiwanja uhamie Buza mkuu
 
Weka bei ya hiyo ardhi yako chap tumalizane.
 
Sasa umenunua kiwanja 32m unakosaje mbavu za kujenga kitu cha maana hata mdogomdogo? Usije ifedhehesha familia yako ukajenga kitu cha ajabu ukawa maskini wa mtaa....wataishi kinyonge maisha yao yote. Mimi nakumbuka enzi za utoto kuna jirani nyumba yao ilikuaga duni afu haikuaga na umeme,mpaka tumekua wakubwa na jamaa wanamaisha yao ila ile picha ya kuwa jamaa walikuaga wanyonge wa mtaa haijapotea..na wao imewaathiri kiaina japo saizi wanamaisha poa walisawazisha baada ya kumaliza vyuo na kupata ajira...na dada yao mkubwa yuko US
 
Haha ninyi ndio mnaponza wenzenu watu humu watadhani mimi kweli wa kishua halafu wakija kunifahamu nje ya jf wanakuta kumbe ni mpuuzi mmoja tu asiye na maajabu yoyote, mkuu trust me mimi siyo wa kishua Mbweni kuna mitaa ni uswahilini typical kama unabisha funga safari uje ujionee hiyo mitaa mwenyewe, mimi wala sina ushua wowote sisi ni masikini wenye unafuu tu wewe ndio unaonekana kwenu wa kishua ila unatuchora tu hapa 😀😀
 
Hapo kwa wanaojenga hiyo mijengo mikali umesahau na wale wazee wanaolala na chatu...
 
Nitakuja ila nitabeba na vyeti kabisa just in case umetupiga kamba hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…