Usiuze wewe jenga kutokana na uwezo wako, watoto wako ndo watafaidi hicho kiwanja na watakushukuru kwa kununua huko.
Usiwe na mawazo ya kuwaza vitu vidogo uwezo wako huo mdogo, do big things.
Tena sisi ambao hatuna pesa, tuna pesa za kudunduliza ndo tunafanya big things.
Miaka mi 3 ilopita nilikutana na ramani mtandaoni nikasema nitajenga nyumba kama hii, ile ramani ni kaliiiiiii balaa akijenga tajiri akakufulu.
2021 hiyo nikaweka msingi tu, nikatulia wakaongea weee ,oh kujidai hii nyumba ataiwezea wapi? Nyumba kubwa kama kanisa yetu macho msingi utamaliza miaka 20🤣 nyumba ina kona kama barabara 😅
Mungu sio ldi juzi nikaenda nikanyanyua nikaipiga lenta mbili, ninavyoongea muda huu majirani hawanisalimii.
Soon naezeka afu natulia niwape nafasi ya kukaa vikao tena. Nahitaji bati kama 150. Maana kutokana na ile design zinakatwa sana.
Sina haraka nikipata laki 5 nafanya kidogo. Hela za kufanya kwa mkupuo sina ila lazima nifike malengo, haijalishi itachukua miaka mingapi.
Sasa wewe umeweza nunua kiwanja mil 32 utashindwa kujenga nyumba nzuri kisa majirani ji mataita?
Unatakiwa kuishi na hao hao la muhimu tafuta ramani nzuri.
Sisi ambao tunadunduliza ndo tunafanya vitu vikali usiogope. Kula kutokana na urefu wa kamba yako.
Mimi sijawahi kuwaza vitu vidogo ningekuwa na hela kama ninavyoona watu wanachezea hela ningefanyaga vitu vikubwa.
N.b usijinyime ukala vibaya kisa unaserv kwa ajili ya kujenga, kula vizuri fanya mazoezi, kunywa maji mengi sana, tumbo mdo tutaenda nalo kaburini, nyumba na magari vitabaki vikigombaniwa dunia.
Mbinguni hakuna hotel.