Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 30,567
- 86,748
Haha sijasema uje kwetu nimesema uje hii mitaa ya uswahilini ili uone kwamba hata Mbweni kuna slums pia 😁😁Nitakuja ila nitabeba na vyeti kabisa just in case umetupiga kamba hapa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haha sijasema uje kwetu nimesema uje hii mitaa ya uswahilini ili uone kwamba hata Mbweni kuna slums pia 😁😁Nitakuja ila nitabeba na vyeti kabisa just in case umetupiga kamba hapa.
Jenga kwa gharama hizo hizoKwa kuanzia kutokana na eneo ni kubwa ningeanza na walau 70M lakini hiyo huku nilipiga tathmini nyumba bei ya chini kabisa ni milioni 300 kuendelea
Kumbe unanusu Eka kabisa tafuta Tajiri akupe 400m
Viwanja vya mbweni watu walishavispot kitambo sana tokea longtimeIko hivi Mkuu, wapiga madili wa nchi hii walishagawana maeneo yao ya kujenga, wale wa kipindi cha nyerere na kuanzia mwinyi wanakaa na wamejenga masaki na osterbay, late mwinyi na kuanzia kwa Mkapa wamejenga Msasani na Mikocheni, late Mkapa na Kikwete wamejenga mbezi Beach na ununio, hawa wa JPM na Mama ndo huko Mbweni sasa. Na wanajenga nyumba kwa miezi mitatu hadi finishing na miti wananunua iliyostawi kabisa hawataki shida.
Sio exactly lakini inakaribiaHiyo nusu?
Jenga kwa gharama hizo hizo
Mbweni JKT kwa ukubwa huo hahizidi 80m kule kwa Mama viwanja vikubwa ndio 200m
Uza hapo hiçho kiwanja pesa utakayopata unañunuwa kiwanja Kinyerezi na unajenga nyumba nzuri Kwa millioni 35 tu.
Hata Mama Samia Private residence yake ni hukohuko Mbweni.
Kuna watu Wana fikra za ajabu sana......yaani unakosaje raha kwa kuwa tu unaishi kwenye makazi duni kwa kujiringanisha na wengine.........??Sasa umenunua kiwanja 32m unakosaje mbavu za kujenga kitu cha maana hata mdogomdogo? Usije ifedhehesha familia yako ukajenga kitu cha ajabu ukawa maskini wa mtaa....wataishi kinyonge maisha yao yote. Mimi nakumbuka enzi za utoto kuna jirani nyumba yao ilikuaga duni afu haikuaga na umeme,mpaka tumekua wakubwa na jamaa wanamaisha yao ila ile picha ya kuwa jamaa walikuaga wanyonge wa mtaa haijapotea..na wao imewaathiri kiaina japo saizi wanamaisha poa walisawazisha baada ya kumaliza vyuo na kupata ajira...na dada yao mkubwa yuko US
Milioni 70 ni pesa ndogo sana kujenga nyumba kwa sasa, ukiniambia pagale nitaakuelewa!!Haina haja ya kuogopa,
Hiyo pesa unaweza kujenga nyumba ya kawaida ila ya viwango ( yenye muonekano mzuri sana )
Tafuta kampuni ya ujenzi nzuri ( Kampuni zipo nyingi sasa hivi na wanafanya kazi kwa ushindani mkubwa ),
Hiyo pesa wanakujengea nyumba ambayo hata hao wanaomiliki mahekalu watatamani nyumba yako hiyo ndogo.
Usiuze wewe jenga kutokana na uwezo wako, watoto wako ndo watafaidi hicho kiwanja na watakushukuru kwa kununua huko.
Usiwe na mawazo ya kuwaza vitu vidogo uwezo wako huo mdogo, do big things.
Tena sisi ambao hatuna pesa, tuna pesa za kudunduliza ndo tunafanya big things.
Miaka mi 3 ilopita nilikutana na ramani mtandaoni nikasema nitajenga nyumba kama hii, ile ramani ni kaliiiiiii balaa akijenga tajiri akakufulu.
2021 hiyo nikaweka msingi tu, nikatulia wakaongea weee ,oh kujidai hii nyumba ataiwezea wapi? Nyumba kubwa kama kanisa yetu macho msingi utamaliza miaka 20[emoji1787] nyumba ina kona kama barabara [emoji28]
Mungu sio ldi juzi nikaenda nikanyanyua nikaipiga lenta mbili, ninavyoongea muda huu majirani hawanisalimii.
Soon naezeka afu natulia niwape nafasi ya kukaa vikao tena. Nahitaji bati kama 150. Maana kutokana na ile design zinakatwa sana.
Sina haraka nikipata laki 5 nafanya kidogo. Hela za kufanya kwa mkupuo sina ila lazima nifike malengo, haijalishi itachukua miaka mingapi.
Sasa wewe umeweza nunua kiwanja mil 32 utashindwa kujenga nyumba nzuri kisa majirani ji mataita?
Unatakiwa kuishi na hao hao la muhimu tafuta ramani nzuri.
Sisi ambao tunadunduliza ndo tunafanya vitu vikali usiogope. Kula kutokana na urefu wa kamba yako.
Mimi sijawahi kuwaza vitu vidogo ningekuwa na hela kama ninavyoona watu wanachezea hela ningefanyaga vitu vikubwa.
N.b usijinyime ukala vibaya kisa unaserv kwa ajili ya kujenga, kula vizuri fanya mazoezi, kunywa maji mengi sana, tumbo mdo tutaenda nalo kaburini, nyumba na magari vitabaki vikigombaniwa dunia.
Mbinguni hakuna hotel.
Dah, halafu ukiangalia mtu hujawahi kumiliki hata 40MNilikwenda kiwanja kinaanzia na million 150 hakuna chini ya hapo huko, ila ukiwa nazo maisha raha sana.
Kwenda jkt ?Unapajua darajani?
Niunganishe na hao jamaaHaina haja ya kuogopa,
Hiyo pesa unaweza kujenga nyumba ya kawaida ila ya viwango ( yenye muonekano mzuri sana )
Tafuta kampuni ya ujenzi nzuri ( Kampuni zipo nyingi sasa hivi na wanafanya kazi kwa ushindani mkubwa ),
Hiyo pesa wanakujengea nyumba ambayo hata hao wanaomiliki mahekalu watatamani nyumba yako hiyo ndogo.