Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Mbweni JKT kwa ukubwa huo hahizidi 80m kule kwa Mama viwanja vikubwa ndio 200m

Mkuu unajua bei za viwanja kweli? Kule kwa Mama viwanja vingi vikubwa vinakaribia ekari moja ,anzia kona ya Mama pale hadi kona ya kwenda baharini ,lile eneo la bara bara ya kwanza hadi ya 6 viwanja ni vikubwa sana ,si chini ya 500m.
 
Usiuze wewe jenga kutokana na uwezo wako, watoto wako ndo watafaidi hicho kiwanja na watakushukuru kwa kununua huko.
Usiwe na mawazo ya kuwaza vitu vidogo uwezo wako huo mdogo, do big things.

Tena sisi ambao hatuna pesa, tuna pesa za kudunduliza ndo tunafanya big things.

Miaka mi 3 ilopita nilikutana na ramani mtandaoni nikasema nitajenga nyumba kama hii, ile ramani ni kaliiiiiii balaa akijenga tajiri akakufulu.
2021 hiyo nikaweka msingi tu, nikatulia wakaongea weee ,oh kujidai hii nyumba ataiwezea wapi? Nyumba kubwa kama kanisa yetu macho msingi utamaliza miaka 20[emoji1787] nyumba ina kona kama barabara [emoji28]
Mungu sio ldi juzi nikaenda nikanyanyua nikaipiga lenta mbili, ninavyoongea muda huu majirani hawanisalimii.

Soon naezeka afu natulia niwape nafasi ya kukaa vikao tena. Nahitaji bati kama 150. Maana kutokana na ile design zinakatwa sana.
Sina haraka nikipata laki 5 nafanya kidogo. Hela za kufanya kwa mkupuo sina ila lazima nifike malengo, haijalishi itachukua miaka mingapi.

Sasa wewe umeweza nunua kiwanja mil 32 utashindwa kujenga nyumba nzuri kisa majirani ji mataita?
Unatakiwa kuishi na hao hao la muhimu tafuta ramani nzuri.

Sisi ambao tunadunduliza ndo tunafanya vitu vikali usiogope. Kula kutokana na urefu wa kamba yako.

Mimi sijawahi kuwaza vitu vidogo ningekuwa na hela kama ninavyoona watu wanachezea hela ningefanyaga vitu vikubwa.

N.b usijinyime ukala vibaya kisa unaserv kwa ajili ya kujenga, kula vizuri fanya mazoezi, kunywa maji mengi sana, tumbo mdo tutaenda nalo kaburini, nyumba na magari vitabaki vikigombaniwa dunia.

Mbinguni hakuna hotel.
Ina sound good, [emoji122][emoji122]
 
Haha ninyi ndio mnaponza wenzenu watu humu watadhani mimi kweli wa kishua halafu wakija kunifahamu nje ya jf wanakuta kumbe ni mpuuzi mmoja tu asiye na maajabu yoyote, mkuu trust me mimi siyo wa kishua Mbweni kuna mitaa ni uswahilini typical kama unabisha funga safari uje ujionee hiyo mitaa mwenyewe, mimi wala sina ushua wowote sisi ni masikini wenye unafuu tu wewe ndio unaonekana kwenu wa kishua ila unatuchora tu hapa 😀😀
Mtoto wa Kishizow kabisa mtu wa maana kabisa!!! Vipi baba hajakupa hela yeyote mama? Hebu angalia pochi basi hio 😂😂😂
 
Usifananishe Masaki na Mbweni utakuwa unajizima data.

Masaki ni prime area nyumba unaweza kupangisha Kwa Kodi kubwà, Nani akapange nyumba Mbweni?
Mbweni Value yake inaelekea huko huko after several years inakuwa kama Masaki tu sababu ya aina ya wakazi waliojenga huko.
 
Mbweni Value yake inaelekea huko huko after several years inakuwa kama Masaki tu sababu ya aina ya wakazi waliojenga huko.
Hakuna kitu kama hiçho na haitokaa itokee.

Masaki ni distance chache Sana kwenda City center.

Master plan ya Darisalama tulishaiharibu, kukaa mbali na City center ni tatizo.

Kutumia masaa mawili ndani ya mji mmoja barabarani ni upuuzi.

Hata unipe free accommodation siwezi kukaa Mbweni never.
 
Habari za Sabato Wakuu!

Wiki nzima hii nilikuwa huku Mbweni, ninakijiplot changu. Sasa kwa hali niliyoikuta nimejikuta ninakata tamaa.

Aiseeh! Hawa majirani zangu sio Pouwa. Hii mijengo walioidondosha na wanaoidondosha sio Pouwa! Unaweza ukadhani upo kwenye filamu za kinaijeria.

Hapa nashauriwa niuze hiki kiwanja kwa sababu pesa ya kujenga vyuma kama vile haiwezekaniki bila kuwa aidha mwekezaji, Fisadi, muuza madawa, mfanyabiashara wa madini, Mwanasiasa mlafi, mzee wa dili haramu na katili, mzee wa kuzamisha wavuni mipira iliyokufa na Watu wa aina hiyo.

Magari yanayopita huku ni magari mazito, Chris Lukosi huita madungu jeshi.

Hivi kweli hawa wanaojenga huku Mbweni ni Watanzania kweli? Maana umaskini wa nchi yetu na hizi nyumba huku ni mbingu na ardhi.

Santeni
uza figo moja ufanye mambo!!
 
UFISADI UNAOSOMWA KWENYE REPORT YA CAG ndio huo Ujenzi unaouona
 
Back
Top Bottom