Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Usiuze wewe jenga kutokana na uwezo wako, watoto wako ndo watafaidi hicho kiwanja na watakushukuru kwa kununua huko.
Usiwe na mawazo ya kuwaza vitu vidogo uwezo wako huo mdogo, do big things.

Tena sisi ambao hatuna pesa, tuna pesa za kudunduliza ndo tunafanya big things.

Miaka mi 3 ilopita nilikutana na ramani mtandaoni nikasema nitajenga nyumba kama hii, ile ramani ni kaliiiiiii balaa akijenga tajiri akakufulu.
2021 hiyo nikaweka msingi tu, nikatulia wakaongea weee ,oh kujidai hii nyumba ataiwezea wapi? Nyumba kubwa kama kanisa yetu macho msingi utamaliza miaka 20🤣 nyumba ina kona kama barabara 😅
Mungu sio ldi juzi nikaenda nikanyanyua nikaipiga lenta mbili, ninavyoongea muda huu majirani hawanisalimii.

Soon naezeka afu natulia niwape nafasi ya kukaa vikao tena. Nahitaji bati kama 150. Maana kutokana na ile design zinakatwa sana.
Sina haraka nikipata laki 5 nafanya kidogo. Hela za kufanya kwa mkupuo sina ila lazima nifike malengo, haijalishi itachukua miaka mingapi.

Sasa wewe umeweza nunua kiwanja mil 32 utashindwa kujenga nyumba nzuri kisa majirani ji mataita?
Unatakiwa kuishi na hao hao la muhimu tafuta ramani nzuri.

Sisi ambao tunadunduliza ndo tunafanya vitu vikali usiogope. Kula kutokana na urefu wa kamba yako.

Mimi sijawahi kuwaza vitu vidogo ningekuwa na hela kama ninavyoona watu wanachezea hela ningefanyaga vitu vikubwa.

N.b usijinyime ukala vibaya kisa unaserv kwa ajili ya kujenga, kula vizuri fanya mazoezi, kunywa maji mengi sana, tumbo mdo tutaenda nalo kaburini, nyumba na magari vitabaki vikigombaniwa dunia.

Mbinguni hakuna hotel.
Samahani mkuu, naeza ona mfano wa ramani hiyo! luckyline
 
Mkuukama hutojali naomba hiyo ramani DM nami nijipe stress nayo. Ahsante
Hii ramani naendelea kuitafuta sikumbuki niliiweka kwenye fail lip, nilihamisha vitu kutoka kwenye sim to pc sasa natafuta bado sijafanikiwa ila nitaipata usijali
 
Mbweni Kijijini ni pale center wanapogeuzia magari ya Makumbusho-Mbweni ,Pale walipojazana wapemba/Mamwinyi ukienda Mbele kuna kamto kamepakana na kambi ya Jeshi - Kiembeni ,Pale hapajapimwa ni slum.
Kote huko napafahamu mkuu huko kote ni mtaa wa Maputo ndio mwisho wa lami, sasa mbona huko kuna afadhali mtaa wa Mbweni ndio asilimia kubwa ni uswahilini na ndio kumejaa wamakonde na hao wapemba unaowasema, viwanja ambavyo havijapimwa vipo hata kwenye mitaa ya ushuani mfano Malindi na Mpiji ni ushuani ila kuna viwanja havijapimwa bado
 
Kote huko napafahamu mkuu huko kote ni mtaa wa Maputo ndio mwisho wa lami, sasa mbona huko kuna afadhali mtaa wa Mbweni ndio asilimia kubwa ni uswahilini, viwanja ambavyo havijapimwa vipo hata kwenye mitaa ya ushuani mfano Malindi na Mpiji ni ushuani ila kuna viwanja havijapimwa bado
Jadda hulali rafiki 🤓
 
Hahaha dah .. we jamaa una maneno hatare! , ni kama wandengereko pia walivyouza maeneo yao huko madale na mivumoni..daah! Leo hii Madale na mivumoni inakuja kwa kasi sana
Hahaha wasichoelewa watu mji unatanukia Goba, madale😂, mbweni kiufupi alongside Bagamoyo Road na huko ni kwa Mid Class Income earners wa kipato cha 50M to 100M annually pamoja na high income earners wa kuanzia 300M na zaidi.


Kilwa road na Pugu road huko ni mchanganyiko wa low class na mid income earners ila kwa ratio wale lower class ni zaidi ya 70 percent. Ndo maana hakuna issue
 
Unapiga kelele sana, unaulizia viwanja na ramani za mbweni halafu huku bonyokwa unataka akae nani 😁
Kaka Mimi sija ulizia kiwanja popote, nili taka kuona ramani ya mkuu luckyline tu.

Beside nataka angusha kidude flani hivi, so nataka nicheki kitu Cha kuni fanya niji tathimini😁.

Beside huko bunyokwa SI uchawini kabisa 😂 Eyce
 
Back
Top Bottom