Hivi huu upuuzi kwenye kazi za ofisini utaisha lini?

Hivi huu upuuzi kwenye kazi za ofisini utaisha lini?

Chief Kumbyambya

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2022
Posts
719
Reaction score
2,408
Bojour wazeeee!

Watu wengine makomwe sana.

Sawa pombe nakunywa ila ni baada ya kazi na kesho on time nimefika jitu linaenda kwenye uongozi wa juu kutangaza aaaah jamaa mitungi saaana wakati sijawahi kufika job nimelewa. au kunywa muda wa kazi. Na uchafuzi wake huu lengo nifukuzwa kazi. Huu ni uchawi grade one na uchawi hauendi kwa mentali(In profesa Jay's voice)

Jitu linanitangaza na kunichafua hivyo wakati nalo usiku tunakutana viwanja ila mi nakuwa na kampani yangu yeye anakula mpweke roho inamuuma kisa ni bosi na hana company alafu mimi surbodnate tu kampani kibao na Ina watu wenye uwezo kuniliko kwahiyo meza yetu huwa nachafukaa balaaaa mavinyaj ya gharama nikiingia viwanja Mimi ni alwatan kuliko yeye.

Nikaona isiwe shida labda kampani yangu inamtisha boss nikawa nahama viwanja mradi tu nisiende pale anapopapenda lakini anauliza watu jamaa Jana alikuwa ananywea wapi mtungi mradi tu anifatilie maisha yangu ya nje ya kazi

Imefika hatua hata kama kuna safari zenye viposho vya hapa na pale jamaa yuko radhi watu wengine waende hata mara nne nne tena ambao kiuwezo na uwajibikaji nimewazidi vizuri hapo Mimi sijaenda hata safari moja(Nazungumzia safari za mikoani maana ndiyo zina posho kubwa) lakini Mimi nauchuna tu kama vile sioni na sijawahi kuhoji Wala nini. I'm just living my life.

Ila hanipati hata kidogo namchora tu mbaya zaidi ni kijana yuko early 40s wala sio mzee ila ana uzee mwingi.

Jana blue monday jioni flani tulivu baada ya kusign out job kanikuta site nafunga king'amuzi cha VALEUR kubwa pembeni na pisi kadhaa kanikata jicha kali sana Mimi ndiyo kwaaaanza namwita mtu wa jikoni alete mdudu kilo mbili na limao za kucheba.

Wewe ni bosi ofisini tuu. Huku mtaani na sisi ni ma Alwattan vilevile a.k.a SENIOR KONTAWA OF THE STREAT.

Stay Tuned Boss. Unapopita napaona.
 
Mabosi wenye wivu, fitina, chuki, hila, n.k ndo walivyo! Yeye anadhani akiwa boss ndo atetemekewe na kila mtu! Mxiuuuh! Hao ni malofa! Ishi maisha yako mwamba ili mradi unatimiza vizuri majukumu ya ajira yako
Ndicho ninachofanya mtungi napiga mbele yake nalala saa tisa usiku na kesho job anawahi ili akute nimechelewa apate sababu ya kusema nachelewa sababu ya mitungi na kulala saa tisa usiku lakini cha ajabu hata awahi vipi ananikuta nishafika kitambo napiga stori na mlinzi nilkiwasubiri wao wafike hapo ndo anapochoka sasa kwamba huyu jamaa ni jini au niaje.😂😂
 
Kama mna clock in muda wa kazi na bado mna muda wa kuwaza na kusemea ya jana jioni bar... Either kazi zenu sio muhimu sana au hamnazo za kutosha.

Na kama baada ya kazi mna muda wa kufuatiliana viwanja, kazi zenu haziwapi changamoto ya kutosha.

Optimization is necessary in any case
Unaishi dunia gani? Hii dunia ione hivihivi kuna binadamu ni afadhali ya nyoka.
 
Back
Top Bottom