Hivi huyo Magoti, mshauri wa Rais kuhusu siasa, alikuwa na uzoefu upi wa mambo ya siasa? Mbona CCM ina manguli wa siasa jamani?

Magu miaka 6, Samia 3 yupo sawa nawe!
Magu hakukaa nae Ikulu 6 yrs, no, Petro alikuwa Makao Makuu ya CCM Dodoma, muda wote alikuwa pale, Magu baada ya kuchaguliwa second term ndio akamchukua kuwa Ikulu, ila hakutangazwa ana nafasi gani pale Ikulu, wala hajawahi pewa barua eti ni mshauri wa Rais siasa etc, alikuwepo kwa kazi wanazojua wao…

So hakukaa 6 yrs na JPM Ikulu, ni kama mwaka hivi or less alikaa Ikulu na JPM
 
MKUUU WAKATI WA MUNGU UKIFIKA HATA HAKUNA AWEZAYE PINGA

MAMAYETU MH SAMIA HAKUGOMBEA NEEMA ZA MUNGU ZIKAMPITIA LEO ANATUONGOZA SAFI KABISA

WEWE UNAWEZAMWONA HAFAI MUNGU AKIAMUA KUKUHESHIMISHA UNAFAA MKUU
 
Live and direct kutoka ikulu! Ww lazma ni wa ikulu.
 
Vyema sana!
 
Ingawa sitaki kusema sio sahihi, ila najua Kuna kitu kinaitwa ofisi ya ushauri kwa Rais maswala ya siasa. Hii ni ofisi yenye watumishi wa Kila namna na wote hujulikana ofisi ya Rais maswala ya siasa. Kama zilivyo ofisi zingine za ushauri kwa Rais. Sina hakika kama yeye ndio alikua in charge Bali alikuwa katika team ya maofisa
 
Naona magoti umeamua kuja kumjibu chiembe 😊😊
 
Mama alikuwa sahihi; kushauriwa na mtu anayejiona ana uwezo mkubwa kuliko wewe ni hatari sana, anaweza kukupa ushauri mbovu ili uharibikiwe.
 
Mkuu umeanza kumjua magoti lini? Pale ikulu yupo muda mrefu...ni very humble guy...labda umemjudge kwa kuangalia physical appearance...Ni mtu muhimu sana kwa Taifa hili...na popote alipo yupo tu kimkakati...
 
Hizo habari za Petro Magoti kuwa mshauri wa Rais upande wa Siasa wewe umezitoa wapi,pamoja na ufuatiliaji wangu wa siasa sijawahi kusikia jambo hilo.
Washauri wa Rais upande wa siasa wanajulikana wapo 4,Lukuvi,Bulembo,Balozi Omar,na Haji kwa maswala ya Zanzibar.
Na kabla hajawateua hawa walikuwepo wengine ambao Magotu hakuwa mmoja wao.

Sasa ww hiyo habari ya magoti umeitoa wapi???????
 
Wewe hujui siasa.
Unafikiri Ile nguvu ya Lowassa ilitokana na nini?
Nguvu ya Kikwete hasa awamu yake ya kwanza ilitokana na nini?
Jibu: Kujiweka karibu na kila makundi ya raia. Wawe daraja la juu, la Kati na la chini Kama wauza madafu na wauza vyakula mitaani.
Kwa hiyo bora Magoti anayetafuta wauza madafu mitaani, a presidential advisor
 
Unafikiri kutumia masaburi na roho mbaya , Magoti ni mtu makini na uelewa mkubwa zaidi ya unavyomjua,
Hana uzoefu wa kushauri ngazi kuu ya taasisi ya Urais.

Wenzetu kule kasome CV ya Condoleeza Rice kabla ya kuwa mshauri wa mambo ya nje wa Marekani. Kwanza alikuwa mhadhiri chuo mambo ya kimataifa, kasoma ana elimu imelala pale, kasoma hadi Urusi pale Moscow State University ajue lugha yao kidogo. Kafanya kazi Foreign Affairs uko Europe kipindi ukuta wa Berlin unaanguka na Soviet Union inavunjika. Baadae ndio akapanda vyeo na kuwa mshauri wa Rais Bush. CV inaeleweka.

Njoo kwa Foreign Minister wa Urusi, Sergey Larvrov, huyu CV imeshiba vilevile. Huyu anajua lugha wanayozungumza Sri Lanka wakati ni lugha ndogo sana.

Sasa njoo bongo, mshauri wa Rais kisiasa hajawahi kuwa hata class monitor. Hata ukimpa uongozi wa kwaya inavunjika
 
Sasa hao uliowataja kuwa wamekomaa kisiasa wameshatusaidia nn?
 
Tambua hii;
Kuna Msaidizi/Wasaidizi wa Rais Siasa...na
Mshauri/Washauri wa Rais ..Siasa..
Kazi za Wasaidizi ni kazi za kuratibu mambo, kwa mfano Rais anataka kufanya mkutano na wanasiasa hawa Wasaidizi watakuwa na jukumu la kuandaa mkutano ikiwemo mialiko,ukumbi na kuchukua mihtasari.
Itakapokuja suala la Rais ataongea nini hapo sasa ndio watakuja Washauri wa Siasa na kumshauri nini cha kuongea/kuzungumza.
Kiswahili kipana sana.
 
Petro alikuwa anakuzwa kisiasa na hiyo nafasi aliyopewa ndio anastahili , kiufupi pale ikulu na makao makuu wapo wengi sana wanakuzwa ili kuja kupewa nafasi .

Ingekuwa ngumu kumtoa from nowhere halafu kumpa nafasi ya ukuu wa wilaya au mkoa .
 
Kwani he was the only one?

Basi mi nilikuwa najua ndio mchawi wao yani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…