Nimeshangaa kusikia Magoti ndiye alikuwa anamshauri Rais kuhusu siasa. Nikimuangalia ni kama ana umri wa miaka thelasini hivi, yaani mtoto tu, na ndio maana mwanzo nilidhani ni mhudumu au afisa wa kawaida tu pale ikulu.
Hivi katika "msitu" wa wazee waliokomaa kisiasa kama Steven Wasira, Mizengo Pinda, Sumaye, Mzee Makamba, Paul Kimiti na wengine wengi kweli Rais anachaguliwa Magoti ambaye hajawahi kugombea hata uenyekiti wa mtaa au kijiji ili akaifahamu siasa kuanzia saiti?
Rais Samia awe anawakataa wasaidizi wengine, asikae nao kwa sababu ya hali zao na huruma tu. Hawa akina Magoti ndio wale wanageuka kuwa madalali wa kumkutanisha Rais na watu.
Nilisikia hata muuza madafu anasema alilipwa na Magoti fedha nyingi ambazo hajawahi kuziona kwa kuuza baskeli chache tu za madafu, sasa hizo nyingi ni nfapi, na kwa nini muuza madafu azione nyingi kuliko mzigo aliouza, na wangapi wanalipwa nyingi, na kwa nini.
Kwa hesabu zozote zile, Magoti is too juniour kumshauri Rais kuhusu siasa, badala yake Rais ndiye anaweza kumshauri Magoti kuhusu siasa. Samia ameogelea katika bahari kuu ya siasa na anagajua mapapa na nyangumi yanayoishi latika bahari kuu ya siasa.
Mh. Rais, usiishie kwa Magoti tu, piga chini wengine wengi ambao "hawajaiva" kumshauri Rais