Hivi huyo Magoti, mshauri wa Rais kuhusu siasa, alikuwa na uzoefu upi wa mambo ya siasa? Mbona CCM ina manguli wa siasa jamani?

Hivi huyo Magoti, mshauri wa Rais kuhusu siasa, alikuwa na uzoefu upi wa mambo ya siasa? Mbona CCM ina manguli wa siasa jamani?

Nimeshangaa kusikia Magoti ndiye alikuwa anamshauri Rais kuhusu siasa. Nikimuangalia ni kama ana umri wa miaka thelasini hivi, yaani mtoto tu, na ndio maana mwanzo nilidhani ni mhudumu au afisa wa kawaida tu pale ikulu.

Hivi katika "msitu" wa wazee waliokomaa kisiasa kama Steven Wasira, Mizengo Pinda, Sumaye, Mzee Makamba, Paul Kimiti na wengine wengi kweli Rais anachaguliwa Magoti ambaye hajawahi kugombea hata uenyekiti wa mtaa au kijiji ili akaifahamu siasa kuanzia saiti?

Rais Samia awe anawakataa wasaidizi wengine, asikae nao kwa sababu ya hali zao na huruma tu. Hawa akina Magoti ndio wale wanageuka kuwa madalali wa kumkutanisha Rais na watu.

Nilisikia hata muuza madafu anasema alilipwa na Magoti fedha nyingi ambazo hajawahi kuziona kwa kuuza baskeli chache tu za madafu, sasa hizo nyingi ni nfapi, na kwa nini muuza madafu azione nyingi kuliko mzigo aliouza, na wangapi wanalipwa nyingi, na kwa nini.

Kwa hesabu zozote zile, Magoti is too juniour kumshauri Rais kuhusu siasa, badala yake Rais ndiye anaweza kumshauri Magoti kuhusu siasa. Samia ameogelea katika bahari kuu ya siasa na anagajua mapapa na nyangumi yanayoishi latika bahari kuu ya siasa.

Mh. Rais, usiishie kwa Magoti tu, piga chini wengine wengi ambao "hawajaiva" kumshauri Rais
Muuaji namba moja kipindi cha magu! usione hicho kibiongo jamaa ni mubaya hatari! |Dracula mnyonya damu
 
Mkuu kwani huyu Waziri fedha wa fedha ana uzoefu gani uliotukuka kuweza kuwa Waziri wa fedha.
 
Hivi Waziri wa Habari sijui bwana Nape ana uzoefu gani huyu na exposure yakuwa pale kwenye ile wizara.?
 
Uko sahihi kwa ulichokiongea, nafasi ni kubwa kuliko uwezo wa mhusika, mshauri wa siasa wa Rais hasa kwa nchi kama Tanzania unahitaji mbobezi hasa aliyekomaa.

Kiuhalisi HAPO NDIO KWENYE FAILURE HASA YA HII NCHI - INCOMPETENCY AND INEXPERIENCE ambavyo vinasababishwa na undugu, ujamaa, ukada, uhawara, udini, ukabila nk
 
Vyeo vinapatikana Kwa connection halafu mnataka mpate positive results, mitaani huku wapo watu wengi sana serious shida ni mifumo.
 
Siyo kila aliyepo nyumba nyeupe ni mshauri wa mambo ya wazi wengine ni washauri upande wa ushirikina na mazindiko.
 
Vyeo vinapatikana Kwa connection halafu mnataka mpate positive results, mitaani huku wapo watu wengi sana serious shida ni mifumo.
Wengine wanapelekwa pale kwa ushirikina na rushwa kusaidia mambo ya wafanyabiashara wakwepa kodi na mafisadi
 
Hana uzoefu wa kushauri ngazi kuu ya taasisi ya Urais.

Wenzetu kule kasome CV ya Condoleeza Rice kabla ya kuwa mshauri wa mambo ya nje wa Marekani. Kwanza alikuwa mhadhiri chuo mambo ya kimataifa, kasoma ana elimu imelala pale, kasoma hadi Urusi pale Moscow State University ajue lugha yao kidogo. Kafanya kazi Foreign Affairs uko Europe kipindi ukuta wa Berlin unaanguka na Soviet Union inavunjika. Baadae ndio akapanda vyeo na kuwa mshauri wa Rais Bush. CV inaeleweka.

Njoo kwa Foreign Minister wa Urusi, Sergey Larvrov, huyu CV imeshiba vilevile. Huyu anajua lugha wanayozungumza Sri Lanka wakati ni lugha ndogo sana.

Sasa njoo bongo, mshauri wa Rais kisiasa hajawahi kuwa hata class monitor. Hata ukimpa uongozi wa kwaya inavunjika

Huku Foreigner affair unamkuta January Makamba, CV yake kafanya kazi Ikulu, kawa Mbunge then Waziri. Halafu eti anakuwa foreigner affair minister.

Mwingine yule Waziri wa fedha, CV yake muajiliwa BOT, Mbunge, Waziri wizara kadhaa then Waziri wa fedha.

Huyu naye ukisoma hapa utaona katika UDSM, UVCCM, IKULU.
Tunachekesha sana.
 
CV inasema kasoma UDSM, then CCM then IKULU, then Uteuzi.

Labda pale Ikulu alikuwa apprentice.
 
Yule Magoti ni miongoni mwa takataka alizoziacha jiwe. Mama imemchukuwa muda kubaini kuwa hii taka ipo ikulu na inakula posho kama mshauri. Alipoibaini kaifagilia mbali, akahangaike na vyoo vya wanafunzi huko
Mwenye macho ambiwi tazama
 
Yule Magoti ni miongoni mwa takataka alizoziacha jiwe. Mama imemchukuwa muda kubaini kuwa hii taka ipo ikulu na inakula posho kama mshauri. Alipoibaini kaifagilia mbali, akahangaike na vyoo vya wanafunzi huko
Mwenye macho ambiwi tazama
 
Mkuu umeanza kumjua magoti lini? Pale ikulu yupo muda mrefu...ni very humble guy...labda umemjudge kwa kuangalia physical appearance...Ni mtu muhimu sana kwa Taifa hili...na popote alipo yupo tu kimkakati...
Naam!
 
Magoti anehitimu pspa 2014 na akina tema tema. Ni mwanafunzi makini wa Dr bashiru.

Alikuwa mwanaccm. Angevaa kijani pekeake coet kwenye foleni ya msosi.

Magoti ni kichwa hasa, Kwa kuwa wengi humu hatuwapendi CCM basi na magoti mwanaccm.

Alikuwa kiongiz tawi la ambiance na seneti.

Aliyemuingiza CCM makao atakuwa nape na makamba kipindi Cha 2011 akiwa chuo na kipindi hicho jalalani ilikuwa chadema yote isipokuwa wachache viongozi wa daruso wengi wao ni viongozi nk.

Alikuwa depo lililofanyiwa usaili TEW April.
Magoti zaidi ya haya ulivyosema mkuu.

Kupanga foleni kwenye misosi alikuwa anawachora tu
 
Back
Top Bottom