Mimi kama nimemuelewa tofauti Joyce anisamehe. Lakini akili yangu inanituma kuamini kuwa baada ya Joyce kuanika sakata hili kwenye media na shutuma alizopata toka kwa wachangiaji, sasa ameamua kuja na episode 2 ili watu wajue chanzo cha ugomvi wao ni ubahili/ubinafsi Wa mumewe na hii anadhani itamsaidia ku atract public sympathy. Lakini ukisoma vizuri maelezo yake unamwonea huruma kwa sababu between lines ameficha tabia yake na anachotaka kiuhalisia toka kwa mumewe. Lakini pia angalau ameeleza chanzo cha kupigwa kwake kuwa ni yeye kwenda "kujirusha" peke yake kama anavyofanya mumewe ili ngoma iwe droo, na anataka jamii ione kuwa kipigo toka kwa mumewe hakikuwa sahihi kwa vile alimkuta sehemu anayoifahamu na hakuwa akifanya zinaa kama yalivyokuwa mawazo ya mumewe. Tatizo la pili la Joyce ni kutofanywa Second signatory kwenye akaunti za mumewe wakati yeye amemfanya signatory kwenye akaunti zake. Katika hili Hoja ya Joy ni ya msingi lakini siyo nzito. Anakiri wakati hili linafanyika hakuona tatizo kwa sababu alikuwa na mapenzi thabiti kwa mumewe. Kwa maana nyingine kinachomfanya ahoji sasa hivi ni kupungua kwa hayo mapenzi thabiti ya awali. Sasa ni kipi kimeyapunguza hayo mapenzi? Ni pale Kilewo alipoacha kumjali na kumthamini, yaani kutoka out peke yake bila mkewe.
Je, haya ni ya kuanika hadharani hata kama kweli yapo? Jibu rahisi ni no, tena big NO! Kinachofanya ayaanike haya kwa sasa ni dhamira yake anayosema alimwambia mumewe tangu mwanzoni mwa mwaka huu, hajataja ni lini, kuwa "MWAKA HUU 2018 NI MWAKA WA KUACHANA".
Huwezi kudumu katika mahusiano kama akili yako umeshaiset kuachana. Ukilala unaota kuachana, ukiamka unawaza kuachana. Siku zote mawazo yanaumba dhamira na mwisho wa siku "UTEKELEZAJI". Joyce unatekekeza ulichokiwaza siku nyingi na sababu ulizotoa ni catalyst. Yaani ulitegesha kama wimbo mmoja Wa Mrisho Mpoto anaposema; "UKINIKANYAGA TU.....!"
Lakini Joy hujachelewa, la kwanza nakusihi acha kutumia njia hii ya kishamba kumdhalilisha mwanaume unayemuita baba Wa watoto wako, na sehemu nyingine umemuita "KILEWO WANGU". Tafuta wenye busara wakusaidie ama KUACHIKA kwa amani au KUREJESHA ndoa yako katika line.
Wasalaam;
Bila bin Bila!!