Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Mhh!mbombo ngafu!Ila Joyce hizo ni siri za ndani na familia yako kwa ujumla hukupaswa kupost huko Insta.Suala kama hili ulipaswa mlimalize kifamilia,je hamna wazazi?ndugu jamaa na marafiki? Unachokifanya ni kujianika kwenye public ambayo kimsingi haina msaada kwenu zaidi ya kukucheka na kukuhurumia kinafiki.
Mumeo hata kama amekosea hukupaswa kuja kulalamika insta,kila mtu akileta matatizo yake insta ndoa nyingi zisingekuwepo.Kama unaona imefika mwisho ni bora uachane naye ,ingekuja tu stori Joyce kaachana na Kileo basi but kwa unachokifanya unajidhalilisha wewe mwenyewe na mumeo!
But pole kwa yote magumu unayopitia tafuta njia sahihi za kumaliza tatizo lenu na sio Instagram.
Ushauri mzuri kama hajachanganyikiwa ataufuata nami ninashauri afuate huu
 
Sisi wahaya huwa tukifikisha umri wa kuoa wazazi hasa mama zetu huwa wanatukalisha chini na kutuhasa kamwe tusioe mwanamke mchagga au mmachame uwa wanatwambia mabaya na madhaifu yao mengi kwenye ndoa ikiwemo hayo yanatokea kwenye familia ya kileo ndo maana ni Nadra sana kumuona muhaya achana na hawa wahaya wasiopajua bukoba,huwezi kukuta kamuoa mtu wa makabila haya....those people are too selfish..!!
Wahaya wanawezana wenyewe kwa wenyewe maana kwa ngono hawajambo.Hata akiwa profesa tabia zake kwenye hio sekta hua ni zile zile kama za ambae hajasoma.

Endeleeni kuoana tu nyie kwa nyie mkuu.
 
Nimeelewa vitu viwili..hii ndoa ilikua ishafeli sasa jamaa alichokifanya ni kuacha kila kitu na kuhama nyumbani...sasa kinachotokea ni frustration za aina nyingi kwa mwanamke maana baba hayupo, gharama zimekua kubwa na jamaa si kuwa hayupo ila pia yupo kimya...ndio maana Joyce anaongea kila mahali maana anahitaji msaada ila hajui aupate wapi, na anaomba aachiwe biashara zake kama biashara nizake kwann aombe aachiwe? Hii ina maana kwamba hizo biashara kafunguliwa na mumewe...kwasasa sina cha kumshauri maana hataelewa...huyo kileo atakua anakaa lodge na hela si anayo ...atatafuta katoto kadogo kakutumbua nae..watoto wake watakua wanateseka mno ila kila akimkumbuka mke atakua anaenda mbali zaidi...natamani ningepata nafasi ya kuwashauri wote...tatizo kileo yupo kimya..hujui na yeye yamemsibu yapi...wanaume wana koromeo...poleni watoto poleni sana...nakaribisha PM kwa ushauri zaidi
Unaakili sana aisee kunywa maji baridi
 
PATA HELA TUJUE TABIA ZA MME WAKO NA KOS HELA TUJUE ZA MKE WAKO.PILI TULISHAAMBIWA TUISHI NA HAWA WATU KWA AKILI HASA KAMA HUYU JOYCE!
 
kupata mtu ambae mna lengo moja nayo changamoto mkuu.kuna watu wabinafsi sana . hv mtu unakuwaje mchoyo hadi kwa damu yako eti.japo tunamuona joyce mbaya ila na huyu kamanda sio kabisa aaah
Umesikiliza upande wa pili weka mizani ndipo utoe hukumu pengine kaamua tu kumzalilisha mwenza kisa kahama nymbn huyu mwanamke sio wa kuolewa hawezi kutunza siri za nymba anatisha kuliko ukoma huyu
 
kumbuka huyu ni mkewe na wana watoto. hapo watoto ukute wakirudishwa ada,hakuna chakula home ,umeme umeisha etc usihukumu mkuu? je kuna mume hapo?
Umemsikia mumewe kajibu nini usitoe haki kwa maelezo ya upande mmoja
 
Swali ni je mitandao ya kijamii kama JF nk. imekuwa mahakimu au wazee wa baraza kuhukumu mambo ya ndoa au kifamilia? Watu wengi huingia humu kuomba ushauri hawaingii humu kung'ong'a wenzi wao. Huyu dada kaja na statement moja kwa moja bila hata kuomba ushauri au kuficha. Kama alivyokuwa naye bila nguo ndo amejivua kwetu sasa hivi.
 
kweli mkuu sku hizi ndoa bhana bora kua singo hayo ni mambo ya ndani sana sio ya kuandika mitandaoni ndoa za siku hizi bana zimekosa muelekeo kabisa inatia kinyaa bora nibaki kua singo duuu
Usikatishwe tamaa na huyu aliye lelewa na tamaduni za magharibi hayo kwao ni kawaida kabisa wapo walio lelewa na maadili yetu ukimpiga akiulizwa anajibu kaanguka kisimani oa tu mkuu muhimu ana maadili ya wapi
 
MKATOE HELA WAKATI HAKUNA! MLIANZA MITANDAONI NA NI LAZIMA MMALIZE MITANDAONI.Superwoman KIRIA.Bado IYOBO na ANTY wake
 
Kieleo nae aje aseme kwa upande wake tuhuma hizi haziwezi kuthibitika ikiwa upande mmoja tu ndio unao lalamika.
 
Mimi kama nimemuelewa tofauti Joyce anisamehe. Lakini akili yangu inanituma kuamini kuwa baada ya Joyce kuanika sakata hili kwenye media na shutuma alizopata toka kwa wachangiaji, sasa ameamua kuja na episode 2 ili watu wajue chanzo cha ugomvi wao ni ubahili/ubinafsi Wa mumewe na hii anadhani itamsaidia ku atract public sympathy. Lakini ukisoma vizuri maelezo yake unamwonea huruma kwa sababu between lines ameficha tabia yake na anachotaka kiuhalisia toka kwa mumewe. Lakini pia angalau ameeleza chanzo cha kupigwa kwake kuwa ni yeye kwenda "kujirusha" peke yake kama anavyofanya mumewe ili ngoma iwe droo, na anataka jamii ione kuwa kipigo toka kwa mumewe hakikuwa sahihi kwa vile alimkuta sehemu anayoifahamu na hakuwa akifanya zinaa kama yalivyokuwa mawazo ya mumewe. Tatizo la pili la Joyce ni kutofanywa Second signatory kwenye akaunti za mumewe wakati yeye amemfanya signatory kwenye akaunti zake. Katika hili Hoja ya Joy ni ya msingi lakini siyo nzito. Anakiri wakati hili linafanyika hakuona tatizo kwa sababu alikuwa na mapenzi thabiti kwa mumewe. Kwa maana nyingine kinachomfanya ahoji sasa hivi ni kupungua kwa hayo mapenzi thabiti ya awali. Sasa ni kipi kimeyapunguza hayo mapenzi? Ni pale Kilewo alipoacha kumjali na kumthamini, yaani kutoka out peke yake bila mkewe.
Je, haya ni ya kuanika hadharani hata kama kweli yapo? Jibu rahisi ni no, tena big NO! Kinachofanya ayaanike haya kwa sasa ni dhamira yake anayosema alimwambia mumewe tangu mwanzoni mwa mwaka huu, hajataja ni lini, kuwa "MWAKA HUU 2018 NI MWAKA WA KUACHANA".
Huwezi kudumu katika mahusiano kama akili yako umeshaiset kuachana. Ukilala unaota kuachana, ukiamka unawaza kuachana. Siku zote mawazo yanaumba dhamira na mwisho wa siku "UTEKELEZAJI". Joyce unatekekeza ulichokiwaza siku nyingi na sababu ulizotoa ni catalyst. Yaani ulitegesha kama wimbo mmoja Wa Mrisho Mpoto anaposema; "UKINIKANYAGA TU.....!"
Lakini Joy hujachelewa, la kwanza nakusihi acha kutumia njia hii ya kishamba kumdhalilisha mwanaume unayemuita baba Wa watoto wako, na sehemu nyingine umemuita "KILEWO WANGU". Tafuta wenye busara wakusaidie ama KUACHIKA kwa amani au KUREJESHA ndoa yako katika line.
Wasalaam;
Bila bin Bila!!
 
Back
Top Bottom