Hivi huyu rafiki yangu anaweza kuwa mtu wa aina gani?

Huyu nini mimi kabisa kila kitu ulichokitaja kinanihusu kasoro hapo hapo kwenye draft,mimi ni mchezaji mzuri wa hilo dubwasha
Unaweza kunifunga mimi ???
 
Huyo ni introvert, watu ambao hawapendi kujichanganya na wengine. Wanapenda kuwa wenyewe kufanya mambo yao kivyao bila kushirikiana na watu.
Wanajichanganya mara chache na wakiona hawakielewi mnachokifanya wanasepa kujitenga.

Huko kusikiliza nyimbo moja kunatokea kwa watu wengi tu hata mimi pia. Kuna siku naamka na mood flan nyimbo ni hiyo hiyo lakini sio kwa siku nyingi kama mwana huyo.
 
Hiyo tabia hata mimi naifahamu mkuu.
Faida zake ni nyingi kuliko hasara kwa sababu kufanya hivyo hujiepusha na mambo mengi na ushawishi mbalimbali.
Watu wa aina hiyo huwa hawapendi makelele kutoka kwa watu wengine kwani huwa inawapa interference.
Faida nyingine ya watu wa hivi huwa wanafocus sana future/long term plans na huwa zinakuja imagination za success kichwani mwao jinsi itakavyotokea in future so kujichanganya na watu huwa wanahisi itamdisturb kisha itamtoa nje ya reli ya mipango yake.
Kutokana na hilo ili kupunguza athari ya upweke alionao ndio anatafuta kitu cha mbadala cha kumliwaza kama mziki ila aupendao ambao utagusa hisia zake na si kila mziki utamfaa,ukimbadilishia mziki usiogusa hisia zake pia atachukizwa na kuhisi makelele.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Uko sahihi mkuu

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Wakati mwingine ni vizuri kujipumzisha ndani kuliko kutoka kisha ukajikuta una tenda dhambi kwa kutazama hivyo vya Nje.

Imagine kumtazama Mwanamke kwa kumtamani umeshazini naye, kumbuka hapo Mjini Wadada wasivyopenda kuvaa nguo za ndani si utajikuta umezini na Dsm yote😜

Ndiyo maana jamaa ana epuka dhambi ndogo nndogo kwa kushinda ndani tu
 
Me naweza kukaa ndani kutwa nzima kila siku
Alafu muziki una hisia sana kama akili yako imetulia na kuusikiliza muziki vizuri utaenjoy sana unaweza kusikiliza tu beat na usizingatie yale maneno au kusikiliza tu maneno ukaachana na beat au pia ukawa unasikiliza feature mbalimbali zilizotengeneza hiyo beat na jinsi zilivyo unganishwa na kuwa beat kamili

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Sasa je hii hali ni kawaida ??.
Hali ya kawaida sana, Sikia huu wimbo, utaachaje kurudia kuusikiliza! ( japo kinachoimbwa hakieleweki)
Your browser is not able to play this audio.
 
Kweli watu na ulimwengu wenu
 
Huyo naye ana watu wanaopenda watu wa hivyo, kwa hiyo kwenye kuoa, anaweza kupatana na mtu anayependa watu wa hivyo.

Hapo ni kama ataamua kuoa, maana anaweza kukataa kuoa, na hiyo ni haki yake pia.
 
Mi nadhani ni kawaida tu mfano mimi toka nimetoka kazini ijumaa nimetoka jana kuangalia mechi ya Manchester basi nimerudi hapa toka niamke sijagusa hata mlango, nimekunywa chai, napika, naangalia movie nalala.

Yani kifupi leo nje sigusi kabisa. Huwa kama sina ishu yoyote sitoki hata mlango sifungui[emoji2].
Labda tuna shida ila naonaga nakua na amani kuliko kutoka huna cha kufanya mkaishia kugombana au kurushiana maneno huko mtaani sipendi. So huwa nadownload movie zangu au series weekend namalizia ndani kama Manchester au simba haichezi sahau kuniona nje.
 
Katika mambo ya imani upo sahihi , ila kumbuka huyu ni mwanaume maisha ya kukaa kaka ndani awaachie wanawake , lakn pia katika mambo ya imani huko huko hakuna jambo (jaribu ) ambalo mwanadamu anakutana nalo likawa nje ya uwezo wake hivyo basi elewa hata hivi vishawishi vyote ulivyovisema au q
uvionavyo vipo ndani ya uwezo wetu katika kuvikwepa .
 
Uzoefu alionao katika jamii ndio chanzo Cha baadhi ya watu kubadilika na kuwa watu wasiopenda kujichanganya mfano,Unaweza Kuta watu wanaomzunguka hawathamini mawazo yake Hali kama hii inaweza kumbadilisha mtu akawa siyo mtu wa kuchanganyikana na watu.
 
Sawa Lakini hebu niambie ungekuwa jobless kama huyu jamaa yangu niliyekusimulia hapo juu je kuishi namna hii uishio wewe ingefaa kweli ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…