Hivi huyu rafiki yangu anaweza kuwa mtu wa aina gani?

Hivi siku hizi kuandika kiswahili watazania sisi kumetushinda kabisa et yani neno mpaka limekua gumu kiasi hiki mpaka liandikwe mbaka?
Yaani kuna maneno yalikuwa yananipa tabu sana humu kuyaelewa ila nimejitahidi kwenda nayo sawa tu hamna namna.

Mtu anaandika;
1. "Ko" akimaanisha "kwa hiyo"
2. "Mbaka" akimaanisha "mpaka"
3. "Make" akimaanisha "maana yake"
n.k.
 
hapa nina gym ina mazagazaga yote,
Your home gym has everything?

Free weights? Machines? Plates? Treadmills? Squat rack? Leg press machine? Angled leg press machine? Calf raise machine? Leg extension machine?

Au unazungumzia mazagazaga yote ‘unayoyahitaji wewe’?
 

Very right, hata mimi ni introvert na huwa nina routine zangu, naamka 2:27am kwa alarm, nalala 7:30pm, huwa niko very strict kwenye hii routine, hata unialike wapi lazima nigeuze kurudi nyumbani kwenye routine yangu.
Sipendi mitoko ya aina yoyote....
 
Unataka akuoe?
 
Unataka akuoe?
 
Uyo jamaa ni kama mimi ila nimebadilika baada ya kuwa na familia na umri kusonga nimejira, imisha kuishi tofauti na ninavyopenda
Kuna washikaji wengi tu uwa wanapenda kuwa karibu yangu lakini nahisi usumbufu, hata iyo hali ya kupenda muziki mmoja ni burudani ambayo utaki ukae mbali nao,
Kiumweli mapokaa pake yangu nainjoy zaidi
Hivi sasa nina watoto ambao nainjoy kuwaona wao tu ma mke wangu ndio rafiki yangu ila nimebadilika siku hizi nimejiforce mpaka ninapenda mpira kuliko ila mautazamia nyumbani kwangu au nikiwa safarini kibiashara nitaenda popote nitazame na eneo ilo nitapata marafiki rakin nitaona usumbufu kuongea
Sipishani sana na uyo jamaa mkuu
Pia sa hivi kuna mitandao so naona mpaka muda hautoshi mashinda mitandaon zaid kuliko kutoka nje na nina injoy life kishenzi
Sina tofaut sana na uyo jamaa ila age yangu imesonga Sana sana
Na niliwah kuishi nje kipindi cha ujana wangu
Tulikamatwa tukafungwa kwangu niliona maisha ya Kawaida tu sikuumia sana kichwa eti nimefungwa au nimamisi kuzurula bali nilikuwa sawa tu mpaka tuliloachiwa mwaka mmoja, nilim mis tu dem wangu,
 
Your home gym has everything?

Free weights? Machines? Plates? Treadmills? Squat rack? Leg press machine? Angled leg press machine? Calf raise machine? Leg extension machine?

Au unazungumzia mazagazaga yote ‘unayoyahitaji wewe’?
Mazagzaga yote is a relative phrase, I am not trying to compete with Schwarzenneger in my home, some stuff I can do at the actual gym.

I have free weights, plates, a treadmill, leg press, multiple multi purpose weight benches, a stationary bike.
 
Mtu unawezaje kuishi katika mfumo huu ?? mimi kwa kweli sipendi mtu anayejitenga tenga bila sababu za msingi hii tabia siyo nzuri maana vingi vitakupita usipokuwa makini
Unaweza kumlaumu ila katika ulimwengu wa sasa watu wamekuwa na mambo ya kipuuzi mengi kuliko ya maana.

Unaweza jichanganya na watu ila story zao sasa, ni Mayele hivi, yanga vile, simba hivi, Arsenal vile. Watu hawana story current za maana zaidi ya kuongea vitu ambavyo havina rutuba katika maisha yao.

Kimsingi kuna watu ni close minded na watu ni open minded. Kukaa na watu close minded ni bora nikaangalie magari barabarani yakiwa yanapita itakuwa burudani na educational zaidi kuliko kukaa na watu wenye fikra za close minded maana naweza gombana nao.

Unakaa na watu ni vilaza, wanashindwa hata kugoogle mambo madogo madogo wanabakia kupinga au kushangaa ukiwa unatoa details ndogo, wanaamini katika kukubaliana kuliko kusahihishana zaidi.

Utasikia "aaaah hapa tunaongea ili kufurahisha jukwaa na akili sio lazima kila kitu mtu uwe unajua" khaaaaaah, hivi kweli, yaani mimi nisikie mtu anakwambia story kama Bill gates ndie tajiri namba moja Duniani halafu nijizuie kumrekebisha, au mtu anaongelea magari halafu anamiss details muhimu nikimjazia nionekane ni much know au mjuaji?

Mwisho wa siku ndio hapo mtu anaona bora akae mwenyewe tu chumbani asome habari mtandaoni ili ajifunze tofauti na akiwa amekaa na watu hawaeleweki kama wachawi.
 
Mmmmmmhmn sasa hii inawezekanaje yaani ukae na watu ambao unaona kabisa ni wazi wapo misinformed na issues mbali mbali za kimaisha then unapishare nao details wao kazi ni kupinga tu sasa unafanya nini na hao watu hapo zaidi ya kupoteza energy yako na kuharibu uwezo wako?

Hii kitu ilimkuta brother yangu, mzee alikuwa anamkanya sana kuwa asiwe na mazoea ya kupenda kukaa na wale watoto wa uswazi sio kwa nia mbaya ila kwa lengo la kumjenga kuwa wale si watu ambao mnafanana nao malengo. Yeye akakaza shingo.

Matokeo yake hawa watu wakaathiri sana saikolojia yake akajiona wale ni wenzake kimaisha. Nadhani unafahamu watoto wa kiswahili life style yao ilivyo simple na huwa inaishia wapi.

Maisha fulani ya kutotaka kujiongeza na kutaka njia za shortcut na gharama nafuu za kuishi. Huyu ndugu yangu akawa mtu wa kuzembea shule, utoro, kujilazimisha kuwa na hobby sawa na hawa watoto wa uswazi ile kutoroka shule kwenda kutazama mpira zile mechi za kombe la bata ila unaona kabisa huyu mwamba hizi sio swaga zake anafosi ili kukubalika.

Mzee alipokuwapo alijitahidi sana kumpiga mikwara ila alipofariki ndio akawa mswahili kabisa. Muda wa chakula anachukua chakula anaenda kulia nje na hao washkaji wa kitaa. Akajiweka mbali na wenzake ambao ndio anafanana nao kimlengo. Wenzake sasa ni wasomi , wengine wahandisi migodini, wengine wakurugenzi halmashauri, ila Yeye sasa kashazingua balaa. Alikuwa anasoma Visiga na hao wenzake wenye mafanikio miaka hiyo ila akawa akirudi likizo anapenda kufosi kukaa na hawa waswahili, matokeo yake discipline yake ikaharibika akashindwa kusoma Visiga boarding ikabidi atafutiwe shule ya Day. Sasa hapo ndipo akazidi kuwa mwehu.

Miaka inaenda leo shughuli zake ni kujichanganya na makonda wa daladala, mara udereva wa daladala, marafiki zake ni wale madalali wa uswazi. Mixer tukaja situka kazaa na mdada wa kiswahili ambaye ana mtoto tayari na ni mama ntilie wale wa uswazi.

Ukikaa nae anaonekana kujutia sana maamuzi yake ya maisha sababu anakumbuka sasa maneno ya mzee alipokuwa akimkanya kuhusu mazoea na kujichanganya na waswahili. Akikutaka na wenzake ambao ndio walikuwa kaliba yake anafanya kuwakwepa maana ni aibu sasa.
 
Nakushuru sana kwa kuweza kushare na mimi sehemu ya historia ya maisha ya kaka yako . Kwa haraka haraka nimeweza kugundua kuwa wewe pamoja na huyu kaka yako mnatokea katika familia ya watu wenye kipato cha katikati au cha juu .

Kwa upande wangu ipo tofauti kidogo , mimi namezaliwa uswazi na kukulia huko , marafiki zangu hata baadhi ya ndugu na marafiki wanizungukao ni watu wenye kipato cha chini , ridhiki na kula yetu inategemeea sana mtu kujichanganya na watu maana kupitia mfumo huo ndyo utapewa mchongo kwamba bwana leo kuna dili huku au kule .

Iringa inashika nafasi ya pili miongoni mwa mikoa inayolima na kutumia bangi kwa kiwango cha juu baada ya Arusha kwa hapa Tanzania . Na moja ya mtaa vijana wanatumia sana bangi , makundi ya hovyo hovyo yasiyokuwa na msingi ambayo yemekuwa yakipelekea matukio ya mauaji karibia kila siku basi ni katika huu mtaa ninaoishi wao wanapaita bondeni au Don south .

Kubwa nalo weze sema hapa ni kijitambua , mimi nimeanza kuiona bangi inavyouzwa na kutumika toka nikiwa darasa la 7 , asilimia 80 ya marafiki zangu wanatumia ila hii haijawahi pelekea nikaitumia ntakaa nao maskani ntapiga nao story muda mwingine nitaenda hata chimbo wanaponyongea ila sijawahi tumia kabisaa ( huwezi amini hili ) .

Siku zote naamini kwenye kile nachokiamini , kama tutapishana mawazo nikawa naujua ukweli nitajaribu kukueleza kwa kile nachokijua ukikataa basi utajua mwenyewe , mfumo huu umenisaidia kuweza kukaa na watu wa aina zote wasomi na hata wasio wasomi na kuniepushia ugomvi usio na ulazima .

Kumbuka napenda mchezo wa draft na ni mchezo unaochezwa sana vijiweni ambako hukutanisha watu wa aina mbali mbali walevi , wahuni , wasomi hata wanasiasa .
 
Yani Toka Jana nausoma Uzi wako mara Tano Tano siamini maana ni kama umenitaja Mimi,anyway Mimi sio nyimbo tu,ila kuna Ile movie ya the gods must be crazy ya bush men,naweza angalia hata mara 5 Kwa siku,na Wala sioni shida.
 
Hapo kwenye muziki ! Muziki ni hisia ! Inaweza kuwa ala au maneno! ndio maana kuna watu wanapenda nyimbo za kongo na wala hawajui kinachoisemwa kwenye bolingo
 
Sioni tatizo na watu ambao tayari mna namna ya kuishi , tatizo ni pale huna maisha hujui pesa utapata vipi afu unajifungia ndani lakin tisa kumi unasingiliza wimbo huo huo tuuu hii maana yake nn ?
Mkuu kulingana na wengine wameshasema wana hali hiyo na imeonekana kama ni hali ya kawaida issue sasa iwe ni wewe kutaka ushauri ufanyeje ili uweze kumshawishi mwanao awe anatoka kujichanganya na wadau mtaani.

Hiyo habari kwanini wimbo mmoja kutwa nzima tuyaache.
 
Pimbi wewe!
 
Mkuu,

Jaribu kujisoma ili ujielewe.

Ila kibongobongo hata kama unatumia mkono wa kushoto na jamii imezoea kutumia mkono wa kulia utaambiwa una majini.

Hatupendi watu kuwa tofauti.


Mkuu unanisema mimi hapa maana ninatumia shot😂😂😂 kipindi nakua mama unajua wazazi wetu tena sijui ni malezi waliyokulia nikipewa kalamu nashika mkono wa kushoto basi nachapwa mkono, nikipewa kitu npokea shoto walichapa mwisho ikashindikana.

Kuna tamaduni za ovyo sana na visheria vya ajabu sana kwangu mimi, mfano mtoto azaliwe nje ya ndoa halafu unasikia mtu mzima anasema mtoto yule haramu🤣🤣🤣huwa nahisi kuchafukwa sana, au kumkataza mtoto kutumia shoto
 
Siku hizi mtu anaweza kushinda ndani, akazurura dunia nzima mitandaoni.

Akawa kafika mbali kifikra kuliko wewe uliyetoka nje.
Kweli kabisa..kwenye muziki kuna ule wimbo wa siku ambao unakuhamasisha kwa siku hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…