Nadhani hii inamuadhiri zaidi mtu anayataka mawazo yake yawe yanakubalika tu kila mara, mimi uwa napenda kuwa free pale tunapojadili mada furani yani kama ntatoa mchango wangu na watu wakaukataa ni sawa, kama ntakuwa na ushahidi juu ya kile nikiongeacho basi ntawaonesha wakikataa tena sina muda wakuendelea kubishana nao na maisha yanaendelea siwezi kaa mbali na watu kisa wanapinga mitazamo yangu
Mmmmmmhmn sasa hii inawezekanaje yaani ukae na watu ambao unaona kabisa ni wazi wapo misinformed na issues mbali mbali za kimaisha then unapishare nao details wao kazi ni kupinga tu sasa unafanya nini na hao watu hapo zaidi ya kupoteza energy yako na kuharibu uwezo wako?
Hii kitu ilimkuta brother yangu, mzee alikuwa anamkanya sana kuwa asiwe na mazoea ya kupenda kukaa na wale watoto wa uswazi sio kwa nia mbaya ila kwa lengo la kumjenga kuwa wale si watu ambao mnafanana nao malengo. Yeye akakaza shingo.
Matokeo yake hawa watu wakaathiri sana saikolojia yake akajiona wale ni wenzake kimaisha. Nadhani unafahamu watoto wa kiswahili life style yao ilivyo simple na huwa inaishia wapi.
Maisha fulani ya kutotaka kujiongeza na kutaka njia za shortcut na gharama nafuu za kuishi. Huyu ndugu yangu akawa mtu wa kuzembea shule, utoro, kujilazimisha kuwa na hobby sawa na hawa watoto wa uswazi ile kutoroka shule kwenda kutazama mpira zile mechi za kombe la bata ila unaona kabisa huyu mwamba hizi sio swaga zake anafosi ili kukubalika.
Mzee alipokuwapo alijitahidi sana kumpiga mikwara ila alipofariki ndio akawa mswahili kabisa. Muda wa chakula anachukua chakula anaenda kulia nje na hao washkaji wa kitaa. Akajiweka mbali na wenzake ambao ndio anafanana nao kimlengo. Wenzake sasa ni wasomi , wengine wahandisi migodini, wengine wakurugenzi halmashauri, ila Yeye sasa kashazingua balaa. Alikuwa anasoma Visiga na hao wenzake wenye mafanikio miaka hiyo ila akawa akirudi likizo anapenda kufosi kukaa na hawa waswahili, matokeo yake discipline yake ikaharibika akashindwa kusoma Visiga boarding ikabidi atafutiwe shule ya Day. Sasa hapo ndipo akazidi kuwa mwehu.
Miaka inaenda leo shughuli zake ni kujichanganya na makonda wa daladala, mara udereva wa daladala, marafiki zake ni wale madalali wa uswazi. Mixer tukaja situka kazaa na mdada wa kiswahili ambaye ana mtoto tayari na ni mama ntilie wale wa uswazi.
Ukikaa nae anaonekana kujutia sana maamuzi yake ya maisha sababu anakumbuka sasa maneno ya mzee alipokuwa akimkanya kuhusu mazoea na kujichanganya na waswahili. Akikutaka na wenzake ambao ndio walikuwa kaliba yake anafanya kuwakwepa maana ni aibu sasa.