Hivi IGP Sirro kwa kauli hii ya Mbowe, Rais Samia, CCM na yote yanayotokea bado haujishtukii tu?

Hivi IGP Sirro kwa kauli hii ya Mbowe, Rais Samia, CCM na yote yanayotokea bado haujishtukii tu?

sasa hivi ziro yupo less less anapeleka dili zake za mwisho mwisho fasta fasta sana, pia anahakikisha ana wa position watu wake maeneo ya uhakika kabla hajatoka
 
Tatizo sio IGP ni mfumo
Kwa mfumo na katiba iliopo, hata akishushwa malaika akapewa u IGP, aratenda chini ya kiwango. Kuwatanguliza wanasiasa na siasa yao kumeharibu mengi.
 
Hii kauli ya Freeman Mbowe kuhusu kushangaa kuwa IGP Simon Sirro mpaka leo yupo ofisini na anashangaa mpaka leo bado yupo ofisini unadhani ni sahihi muda huu mkuu huyo wa Jeshi la Polisi anatakiwa akuwa ameshajiuzulu...
Tukisema polisi akili zao wanazijua wenyewe tunasimangwa tunaambiwa polisi ni wasomi hamna mfano, haya sasa
  1. Rais ameingiwa shaka na utendaji wa jeshi ie kiongozi wake ni kama hayupo
  2. Chama kinacholelewa na jeshi nacho kimelalamikia jeshi implication ni kwamba jeshi halina kiongozi
  3. Wanaovaa kaki kama jeshi kasoro kofia nao wanalalamikia jeshi lakini kiongozi ametia pamba masikioni
  4. Polisi wenyewe wameuambia umma hadharani Mtwara kwamba ni majambazi walioko kwenye ajira lakini kiongozi yupo tu
Akili ya kujihuzuru hana wala hana mshipa wa aibu
 
Mwenyekiti wa CCM ndiyo anapenda Sirro aendelee kuwa ofisini kwasababu CCM bila polisi haina uwezo wa kushinda.
Alinukuliwa akisema hatuwezi kutawaliwa na ma,/gaidi kipindi kile cha kampeni. Juhudi zake zilikipa nguvu ccm na kudhoofisha vingine. Dola ni mfungamano...
 
"huwa wana semaga ni upepo tu utspits"

Bila shaka sirro na simama upepo upite.

Haina aibu
 
Hii kauli ya Freeman Mbowe kuhusu kushangaa kuwa IGP Simon Sirro mpaka leo yupo ofisini na anashangaa mpaka leo bado yupo ofisini unadhani ni sahihi muda huu mkuu huyo wa Jeshi la Polisi anatakiwa akuwa ameshajiuzulu...
Kipindi cha Magufuri, mlikuwa mnasema Magufuli ndiye anayeua, sasahivi Magufuri hayuko kuna Samia mnasema mnasema Siro ndiye anayeua,🤣🤣🤣hata hatawale malaika mauaji hayawezi koma mladi wahalifu wanazaliwa kila Siku,sawa polisi wanasehemu yao lakini matatizo mengine tunayaleteleza sisi kwa kutokufuata sheria na taratibu za nchi.
 
Huyu baba anaroho ngumu y dunia, watu wazima tukivuliwa hua tunachutama
 
So tatizo la polisi limeanza na Siro. Huyu kiongozi alikuwa mtu fighter sana wa maovu mipakani. Leo mnakunyaaaa kwa Amani sababu Yake na wengine. Wema wapo na wabaya wapo. Hata wewe una mabaya yako. Mema yao yanazidi mabaya na ndo mana tunaishi.
Wakikutembelea ndiyo utaufahamu uzuri Wa Polisi Wa Tanzania chini ya Sirro Wa CCM.Kwa Sasa unaruhusiwa kumsifia Sirro kwa kutulinda na kutokutuua kwa wingi.
 
Hiyo culture ya kujiuzulu mara zote uwa inajengwa. Na misingi yake inajikita kwenye KATIBA BORA.

Nadhani pointi yako ya msingi isiwe kushangaa bali iwe kuhitaji mabadiliko makubwa sana ya KATIBA.

Yanayofanyika nchini/serikalini yangekuwa yanafanyika ndani ya Klabu ya Simba au Yanga nadhani yangezungumzwa na kulalamikiwa chini na angani, nchi kavu na baharini!

KATIBA BORA haikwepeki!
 
Siro kingai mahita jumanne gudlack sijui wanajisikiaje kumuona waliyembakika kesi ya ugaidi akiwa huru
 
Hii kauli ya Freeman Mbowe kuhusu kushangaa kuwa IGP Simon Sirro mpaka leo yupo ofisini na anashangaa mpaka leo bado yupo ofisini unadhani ni sahihi muda huu mkuu huyo wa Jeshi la Polisi anatakiwa akuwa ameshajiuzulu...
Alikuwa na kesi ya kujibu kwanini a jiuzulu.
 
Hii kauli ya Freeman Mbowe kuhusu kushangaa kuwa IGP Simon Sirro mpaka leo yupo ofisini na anashangaa mpaka leo bado yupo ofisini unadhani ni sahihi muda huu mkuu huyo wa Jeshi la Polisi anatakiwa akuwa ameshajiuzulu...
Mbowe ni nani kwenye serikali? mbowe akisema au akishangaa sirro bado ni IGP italeta madhara gani kwa taifa. mbona watu wanamshangaa yeye mbowe bado tu mwenyekiti miaka nenda rudi why?
 
Madaraka matamu jamani

Mbowe anamshangaa Sirro kuwepo madarakani ilhali yeye Mbowe ana takribani miaka 17 sasa bado kang'ang'ania uenyekiti wakati CCM kwa miaka hiyo tayari walishakuwa na Mkapa, Kikwete, Jpm na sasa Samia

Na bado Mbowe alifanya figisu kwa kunyofoa kipengele cha katiba kilichokuwa kimeweka ukomo wa kuongoza madarakani ndani ya Chadema
 
Tatizo sio IGP ni mfumo
Inawezekana kabisa tatizo ni mfumo, hasa wa kumpata IGP!!lakini jeshi limekuwa la kulaumiwa sana hasa awamu ya 5, baada ya kuonekana rais analiunga mkono kwa kila kitu wanachokifanya hata kiwe kibaya!!kama kipindi kile cha omary mahita, alipokuja said mwema akaliweka jeshi kwenye mstari, ila daa kwa sasa ni balaa!!na ni kutokana na wanasiasa!!Mama atafute tu IGP mpya tena itapendeza aweke mwanamke tu, huyu wa sasa hamna kitu, aliwezana na upepo wa jiwe ,
 
Madaraka matamu jamani

Mbowe anamshangaa Sirro kuwepo madarakani ilhali yeye Mbowe ana takribani miaka 17 sasa bado kang'ang'ania uenyekiti wakati CCM kwa miaka hiyo tayari walishakuwa na Mkapa, Kikwete, Jpm na sasa Samia

Na bado Mbowe alifanya figisu kwa kunyofoa kipengele cha katiba kilichokuwa kimeweka ukomo wa kuongoza madarakani ndani ya Chadema
Kwa akili zako unafikiria kuwa mwenyekiti wa chama cha upinzani kwa nchi za kiafrika ni sawa na kuwa mwenyekiti wa chama tawala?!
Lazima uwe umejitolea maisha yako, ni wa ngapi wako tayari kuona wanafirisiwa mali zao?!jela kila leo, nenda uganda kwa dk.kiza besigye, zimbambwe kwa marehemu morgan changilaye.

Hao kina Nyerere, mujoma, Neto, samora, Mandela, wangetumia njia hiyo wasingefika hapo walipofika kupigania uhuru wa nchi zao!!
Mbona hao viongozi wa ccm wanapokuwa madarakani hawataki kusikia kabisa habari za kutenganisha kofia?!!
 
Hii kauli ya Freeman Mbowe kuhusu kushangaa kuwa IGP Simon Sirro mpaka leo yupo ofisini na anashangaa mpaka leo bado yupo ofisini unadhani ni sahihi muda huu mkuu huyo wa Jeshi la Polisi anatakiwa akuwa ameshajiuzulu...
Kama hakujiuzuli kwenye sakata la MO , usitegemee ajiuzulu leo
 
Yaani Mbowe akishangaa ndio IGP Siro ajiuzulu? Mbowe ni nani nchi hii?

Watu wengine sijui akili hua mnatumia kufanyia nini maana inaonyesha wazi hamtumii akili kufikiri.
Wewe ndio hufikiri,Mbowe ni nani?

Uliwahi sikia wapi mtuhumiwa wa ugaidi mwenye ushahidi wakutosha anaakikwa Ikulu.

Uliwahi sikia wapi Duniani mtuhumiwa wa ugaidi anawavuta mabalozi kusikiliza kesi za ugaidi.

MBOWE ni sehemu ya Umma wenye sauti ndani na nje ya Nchi.
 
Back
Top Bottom