Mtambachuo
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 2,919
- 5,558
Duh.... mtu mfu hajui neno lolote... ila sio mbaya kama mtu amechagua kuchomwa akifa hakuna shida!!! kikubwa awe ametubu na kuiamini injili
Tajiri binadamu ni huru, anatumia uhuru huo (madam havunji sheria) kuamua mambo yake (kwa sababu zake), akiwa hai na akiwa amekufa.
Kwani marehemu anaamua kuandika katika wosia wake, akazikwe sehemu flani inakuwa ni matakwa yake.
Hivyo basi hata cremation ni matakwa ya marehemu. Ni vile anavyoona yeye inafaa (awe sahihi au asiwe sahihi)
Mfano; Wangali Mathai mwanaharaki wa mazingira Kenya, aliandika katika wosia/will kwamba akifa achomwe sababu aliona kwamba, yeye kuzikwa ni uchafuzi wa mazingira na ekolojia.
The same story; Ngugi Wa Thiong'o aliweka katika exile kwa miaka mingi nje ya nchi yake ya Kenya. Aliacha wosia kwamba akifa asizikwe Kenya, bali achomwe moto na pasiweko kaburi lake popote. 😊
Kinachomuona Mungu ni roho na siyo mwili
Binafsi napendelea cremation, hata nikifa kesho au keshokutwa ningependelea cremation, majivu hata wakitupa mtoni siyo mbaya, mtu ukishakufa unareturn kwenye non existence, neuronal activity za kwenye brain ziki shut down , moyo ukastop na Kila organ ikafa hausikii chochote hata wakinichoma haitanisumbua, kuzika kwa makaburi kunakula nafasi sana, miaka inavyoenda tutakosa sehemu za kuzikia.
Cult ni nini ?Hili la mtu kuchomwa baada ya kufa sio common sana kwa Afrika lakini kuna baadhi ya Waafrika eti akifa anachagua kuchomwa badala ya kuzikwa mwili mzima.
Mimi hii naiona kama cult kwa sababu hainiingia akilini kuona mtu anachagua kuchomwa, badala ya kuzikwa ambayo mwili mzima kama ilivyo asili yetu.
Ina sound kama satanic hivi ? na sijui utaratibu ukoje kwa viongozi wa dini Wakristu na Waislam huwa wanalichukulia vipi pale mmoja wa muumin wao anapochagua utaratibu huu wa kuchomwa au wengi wao wanakuwa ni Atheists. Hii hata tamaduni zetu za kimakabila zinakata kabisa.
Utajisikiaje au utachukuliaje mtoto wako au ndugu yako anapochagua kuwa cremated..?
Ukizikwa unaenda na ndugu kaburini?Sawa ila huoni kama inaenda kinyume na tamaduni zetu na zoezi lenyewe linawetenga hata ndugu.
Cult ni nini ?
Najua hawatapenda kwasababu ya tamaduni na desturi ila mimi nikiulizwa kati ya normal burial na cremation baada ya Kifo changu, ningeenda direct kwenye cremation, ile ni fasta masaa kadhaa mzoga wako unakuwa majivu habari inaisha hivyo, kuliko kuzikwa na mijeneza unaoza mdogo mdogo mpaka uje kuwa skeleton ni miaka 15+, bora hata waislamu hawaziki na jeneza unaoza chap na kuwa skeleton hapo hapo, ila cremation ni quick and fast , ina save space and timeDah unatisha sana, unadhani ndugu zako wanapenda huo utaratibu.
Ukizikwa unaenda na ndugu kaburini?
Ni uhuru wao mkuu lakini naona ipo tofauti na tamaduni zetu za Kiafrika na ni jambo linalotisha.
Najua hawatapenda kwasababu ya tamaduni na desturi ila mimi nikiulizwa kati ya normal burial na cremation baada ya Kifo changu, ningeenda direct kwenye cremation, ile ni fasta masaa kadhaa mzoga wako unakuwa majivu habari inaisha hivyo, kuliko kuzikwa na mijeneza unaoza mdogo mdogo mpaka uje kuwa skeleton ni miaka 15+, bora hata waislamu hawaziki na jeneza unaoza chap na kuwa skeleton hapo hapo, ila cremation ni quick and fast , ina save space and time
Uhuru wa mtu sio lazima uwe na uhalisa. Kwa mfano wewe unaweza kuwa vegetarian/huko nyama. Ni uhuri wako binafsi madamu huvunji sheria.
I prefer kuchomwa kuliko kufukiwa ukiwa na mwili hivi dah
Mungu yupi ?Ni imani ambayo ipo kinyume na imani ya Mungu