Nimekuelewe na umechambua vema lakini kani sehemu alipozikwa mtu baada ya miaka mia moja kuna shida gani akizikwa hapo mwingine...?
Nakubaliana na kuchukua vya wengine lakini visivyofaa au vinavyokinzana tamaduni na taratibu zetu si vema kuzichukua.
Vipi huko ughaibuni ulipo ni asilimia ngapi wanachomwa....?
Ukifuata hayo mambo ya asili, alipozikwa mtu ni sehemu yake ya mwisho ya kupumzika, hatakiwi kuzikwa mwingine. Hapatakiwi kusumbuliwa, hapatakiwi kuchimbwa wala kujengwa kitu kingine zaidi ya kaburi.
Mimi nimesoma Muhimbili Shule ya Msingi pale, hii barabara ya Maliki inayokatiza kutoka Don Bosco chini huku kupandisha kwenda Muhimbili Hospital zamani ilikuwa haipo, palikuwa na makaburi pale.
Sasa serikali ikaona kuna haja ya kupitisha barabara pale, kurahisisha kufika hospitali kutoka huku Upanga chini.
Kukawa na mgogoro mkubwa sana. Kwa sababu pale kuna makaburi ya kina Jumbe Tambaza watu wamezikwa kabla Sultan Majid hajaanzisha Dar es salaam. Kina Jumbe Tambaza ndio wazee wenye mji hao waliomuuzia Sultan Majid ardhi akanzisha Dar es salaam.
Ikabidi watu waelezwe umuhimu wa barabara, waelezwe kuwa makaburi yatachimbuliwa na miili kuzikwa tena pembeni kwa heshima zote.
Wengi walipinga mpaka mwosho. Ulikiwa mzozo mkubwa sana Msikiti wa Tambaza pale.
Ndiyo pakachimbwa upya barabara.
Sasa ilikuwa tabu sana, ulikuwa mzozo, ilitakiwa extra effort, ambayo isingetakiwa kama watu wasingekuwa wamezikwa.
Ukisema ukubali alipozikwa mtu baada ya muda azikwe mwingine tayari ushakiuka tamaduni nyingine, sasa kwa nini ukatae kukiuka kuchoma moto?
Hii ni habari ya kukumbatia mambo kwa logical fallacy ya "argument from tradition".
Ni habari ya kusema "Tunafanya hivi" ukiulizwa, kwa nini? Unajibu "Kwa sababu tumekuwa tukifanya hivi".
Ukiulizwa "Kwa nini tumekuwa tunafanya hivi na si vinginevyo?:
Unajibu "Basi tu, ndiyo utamaduni wetu".
Lakini hata utamaduni unabadilika.
Makabila mengi kulikuwa na utamaduni wa kutahiri wanawake, sasa hivi unatoweka.
Utasema tuendelee kutahiri wanawake kwa sababu ni utamaduni wetu tu?
That is "argument from tradition" logical fallacy.