Hivi inakuaje mtu anachagua akifa achomwe (Cremation) mimi huwa naona kama ni Cult

Hivi inakuaje mtu anachagua akifa achomwe (Cremation) mimi huwa naona kama ni Cult

Najua hawatapenda kwasababu ya tamaduni na desturi ila mimi nikiulizwa kati ya normal burial na cremation baada ya Kifo changu, ningeenda direct kwenye cremation, ile ni fasta masaa kadhaa mzoga wako unakuwa majivu habari inaisha hivyo, kuliko kuzikwa na mijeneza unaoza mdogo mdogo mpaka uje kuwa skeleton ni miaka 15+, bora hata waislamu hawaziki na jeneza unaoza chap na kuwa skeleton hapo hapo, ila cremation ni quick and fast , ina save space and time
Kuzikwa mara wachawi wafukue mwili wafanyie yao
 
Ukifuata hayo mambo ya asili, alipozikwa mtu ni sehemu yake ya mwisho ya kupumzika, hatakiwi kuzikwa mwingine. Hapatakiwi kusumbuliwa, hapatakiwi kuchimbwa wala kujengwa kitu kingine zaidi ya kaburi.

Mimi nimesoma Muhimbili Shule ya Msingi pale, hii barabara ya Maliki inayokatiza kutoka Don Bosco chini huku kupandisha kwenda Muhimbili Hospital zamani ilikuwa haipo, palikuwa na makaburi pale.

Sasa serikali ikaona kuna haja ya kupitisha barabara pale, kurahisisha kufika hospitali kutoka huku Upanga chini.

Kukawa na mgogoro mkubwa sana. Kwa sababu pale kuna makaburi ya kina Jumbe Tambaza watu wamezikwa kabla Sultan Majid hajaanzisha Dar es salaam. Kina Jumbe Tambaza ndio wazee wenye mji hao waliomuuzia Sultan Majid ardhi akanzisha Dar es salaam.

Ikabidi watu waelezwe umuhimu wa barabara, waelezwe kuwa makaburi yatachimbuliwa na miili kuzikwa tena pembeni kwa heshima zote.

Wengi walipinga mpaka mwosho. Ulikiwa mzozo mkubwa sana Msikiti wa Tambaza pale.

Ndiyo pakachimbwa upya barabara.

Sasa ilikuwa tabu sana, ulikuwa mzozo, ilitakiwa extra effort, ambayo isingetakiwa kama watu wasingekuwa wamezikwa.

Ukisema ukubali alipozikwa mtu baada ya muda azikwe mwingine tayari ushakiuka tamaduni nyingine, sasa kwa nini ukatae kukiuka kuchoma moto?

Hii ni habari ya kukumbatia mambo kwa logical fallacy ya "argument from tradition".

Ni habari ya kusema "Tunafanya hivi" ukiulizwa, kwa nini? Unajibu "Kwa sababu tumekuwa tukifanya hivi".

Ukiulizwa "Kwa nini tumekuwa tunafanya hivi na si vinginevyo?:

Unajibu "Basi tu, ndiyo utamaduni wetu".

Lakini hata utamaduni unabadilika.

Makabila mengi kulikuwa na utamaduni wa kutahiri wanawake, sasa hivi unatoweka.

Utasema tuendelee kutahiri wanawake kwa sababu ni utamaduni wetu tu?

That is "argument from tradition" logical fallacy.

Tunashukuru kwa historia nzuri hatukuwa tunaijua

Ila tamaduni nilizosema ni zile nzuri ndio tuziendeleze.

Jua kuna watu ambao ni Wahafidhina/ traditionalist na wengine ni Liberal kwa hiyo huo utaratibu wa kuchoma hata kama una manufaa bado kwenye jamii yetu hatuukubali.
 
Dunia ina miaka zaidi ya Milioni, maisha yameanza zaidi ya Maelfu ya miaka BC na mpaka leo hii binadamu hana uwezo bado wa kujaza ardhi yote kwa 100%, nafasi iliyopo ni kubwa maelfu ya miaka ila bado nafasi za kuzikia zipo,

cha ajabu kizazi chenye miaka 2000 tu ndo kinasema eti Kuzika watu kutafanya dunia ijae nafasi.

Ajabu kaka na mimi nashangaa wanatafuta sababu za kujustify ambazo hazina uzito na istoshe mwili wa mwanadamu sio plastic anaoza.
Ni nafasi kubwa kiasi gani mtu anachukua anapozikwa.
 
Binafsi napendelea cremation, hata nikifa kesho au keshokutwa ningependelea cremation, majivu hata wakitupa mtoni siyo mbaya, mtu ukishakufa unareturn kwenye non existence, neuronal activity za kwenye brain ziki shut down , moyo ukastop na Kila organ ikafa hausikii chochote hata wakinichoma haitanisumbua, kuzika kwa makaburi kunakula nafasi sana, miaka inavyoenda tutakosa sehemu za kuzikia.
Hutaki watoto na familia wawe wanatembelea kabuli lako?...
 
Back
Top Bottom