Shukuru sana Mungu kukuepusha na jaziba kuliko hayo mengine yaliyofuatia.
Mtu yeyote anapolewa akili hupungua uwezo wa kufanya kazi.
Kwa hiyo tabia chafu aliyokuonesha, saazingine si yake kwa kujiona yeye yupo juu ya kila mtu.
Ungeiruhusu hasira ikutawale, yawezekana muda huu usingeliweza kuandika hata hii thread kutokana na kibano mbacho ungelikuwa ukikipata aidha kwa kuua au kujeruhi, maana walevi wengi hufa kirahisi sana kutokana na kinga zao za mwili kuwa zipo chini.
Nasema tena ulitumia busara kubwa sana kuizuia hasira yako, pia jiepushe kupitia sehemu za walevi kama wewe mwenyewe hautumii pombe.