Pre GE2025 Hivi inakuwaje CCM imara kabisa itumie njia za gizani gizani kushinda uchaguzi!?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM ni ileile
 
CCM ni chama dhaifu kabisa ambacho hakiwezi kushinda uchaguzi wowote bila mbeleko ya vyombo vyote vya dola. Kingekuwa imara wangeweka uwanja sawa ili wapiga kura ndiyo waamue. Kitendo cha kuitumia Tamisemi kuengua wagombea wa upinzani ni ishara ya wazi ya woga wa CCM kushindana na wapinzani wake kisiasa.
 

Attachments

  • JamiiForums-979014263.jpeg
    63 KB · Views: 1
Mlisimamisha wagombea wangapi nchi mzima?
Sidhani kama mmefika hata 10%

Hamuwezi kuwa wapinzani Kwa kelele za mitandaoni wakati wenzenu wapo on the ground
Wewe taarifa za kwamba wapinzani wamesimamisha wagombea 10% ulizipata wapi kama siyo mitandaoni?
Unaishi wapi hapa Tanzania? Unalijua lilipo jimbo la kawe? Unajua population characteristics zake? Unakubali kwamba wagombea wote jimbo la kawe walikuwa hawana sifa na wale wote wa ccm kutoka jimbo la bumbuli wanazo sifa?
Unamjua mwenyekiti anayeitwa huru wa kamati ya rufaa? Ni nani kwa cheo? Das anapatikanaje?
Tuache unafiki! Tuwe wakweli bila dola ccm haiwezi.
Mwaka mmoja huko Tanganyika nilipanda gari ya DSO lift. Ilikuwa ni uzinduzi wa kampeni za ccm. Ndani ya ile gari yule mzee alikuwa amepakia madera, khanga na tshirts ya ccm kwa ajili ya kuwagawia watu na huku anauliza kwa simu " mtaa fulani mmeshawapa"?
Huyo ni afisa usalama wa wilaya halafu anatokea mbwiga mmoja anasema gentleman siasa ni kujipanga?
 
CCM ni weupe kabisa hawana uimara wanaotupigia kelele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…