Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

😀😀😀😀😀Mkuu mada umeielewa lkn
 
Hata mama nitilie anatumwa na walaji, mfuga kuku anatumwa na wateja wake, President, Mawaziri na wabunge wote wanatumwa na wananchi. Embu tueleze kazi unayofanya wewe hiyo ni ya namna gani, Au unafanyia mbinguni?
 
Wakati unajiuliza hilo, hukujiuliza inakuwaje unatumia Mtandao wa Jamii Forums aliobuniwa na mtu mwingine na sio wewe?
 
Hapo unawatumikia binadamu na mifugo ili uweze kuishi
Hapana nafanya shughuli zangu mwenyewe kwa uhuru bila kusimamiwa na mtu. Wewe uliye ajiriwa hapo unamwogopa boss kila ukimwona tu unahisi kufokea au kufukuzwa kazi. Sasa mimi naweza kumhofia mteja wangu kwa lipi mkuu.
 
Nmejaribu kuwaza tuu wanajeshu nao wajiajiri na mapolisi na matrafiki na manesi na madakatar na malecture nao wajiajiri ......ongezea na wengne
 
Umenena vyema. Wapo watu wameajiriwa na wanavuta mkwanja wa maana wanawashangaa watu kwa nini wanahangaika na biashara. Vice versa is true.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…