Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Tofautisha Kati ya kuajiriwa na kujiajiri, vinginevyo rudia tena kusoma uzi,kina maeneo hujayaelewa.
Nakwambia hivi, hata unaposema umejiajiri, bado umeajiriwa.

Mathalani, anayesema amejiajiri kwa kunzisha biashara naye inambidi awe na good customer service kuwavutia wateja, hapo na yeye kaajiriwa na wateja anafanya kazi kuwavutia wateja.

Hilo moja.

Pia, ikiwa kila mtu atataka kujiajiri, hakuna atakayeweza kujiajiri.

Kwa sababu hao wanaojiajiri pia wanataka watu wa kuwaajiri, wanataka mifumo ya kiserikali ambayo ina watu walioajiriwa.

Kwa hiyo, ni ushamba na ufupi w amawazo kutaka kila mtu aajiriwe au kila mtu ajiajiri.

Sasa kuna mtu ndoto ya maisha yake yote ni kuwa Jenerali wa Jeshi la Tanzania.Ailinde nchi yake kwa kuwa mwanajeshi mwenye ushawishi mkubwa.

Sasa huyu naye unataka ajiajiri vipi wakati kuwa Jenerali wa Jeshi la Tanzania inabidi uwe muajiriwa wa serikali ya Tanzania kwa miaka mingi?

Unataka kusema watu wote wanaotaka kutumikia nchi yao kwa kuajiriwa serikalini hawana akili timamu?

Kwa nini unafanya unachotaka wewe ndiyo kiwe kitu cha akili timamu, na wanachotaka wengine si cha akili timamu?

Hao ma genius wakina Einstein walioajiriwa kufundisha vyuo vikuu na kufanya research wote hawakuwa na akili timamu?

Robert J Openheimer alivyoendesha Manhattan Project na kuvumbua bomu la atomiki alifanya kazi ya kuajiriwa na serikali, naye hakuwa na akili timamu?
 
Umeanza kuvuta bangi lini mkuu?
 
Ukimsoma anamaanisha kujiajiri na sio kuajiriwa. Anaamini kujiajiri ni maisha mazuri zaidi.
 
Mimi nawajua watu wana makampuni yao, wamejiajiri.

Wanafanya biashara ya kufuata "tender process", kupata biashara za serikali.

Wanawanyenyekea kichizi waajiriwa wa serikali wanaopitisha nani apate tenda na nani asipate tenda.

These things are not as simple as nani kaajiriwa na nani kajiajiri.
 
Mkuu umenena kila kitu...Zamani sana nikiwa kijana nakua nilidhani ukijiajiri ndio unakuwa stress free na kuenjoy life....ebwanaeee, nimekutana na maboss wana stress ya kazi za wateja wao...Mteja ni mfalme..maboss wanafanya kazi za wateja..kiufupi tunategemeana katika circle structure kiasi kwamba kila mtu ni Boss wa mwenzie...
 
Hivi mtu uliyeajiriwa kwenye ofisi ya mtu unaweza wekaa miguu kwenye meza, unaweza kuamua kuchelewa kazini. Muda wote unaogopa boss wako
 
Wakati huo wanadanganyana kwa kujiita ma CEO wakat hata genge la nyanya hawana.
Yani hawa vijana nj changamoto tujifunze kuishi nao tu.
Yani mtu analeta mada ila unaona kiukweli huyu mtu hana uelewa wa kitu anachokiongea ye anIshi kwenye fantasy tu.
 
Hapana nafanya shughuli zangu mwenyewe kwa uhuru bila kusimamiwa na mtu. Wewe uliye ajiriwa hapo unamwogopa boss kila ukimwona tu unahisi kufokea au kufukuzwa kazi. Sasa mimi naweza kumhofia mteja wangu kwa lipi mkuu.
Vipi ulifanikiwa kupata kazi make kuna uzi humu unalia njaa sana.
 
Umenena kweli....mwanzo nilijua unatuzodoa lakini uliposema baada ya miaka mitano ndio nikaelewa una point muhimu.


Antony Mtaka alisema, " Nawaheshimu mno sector binafsi kwa sababu kujiajiri sio kitu rahisi hata watumishi wa Umma wenye mishahara zaidi ya 2M wanashindwa kujiajiri " mwisho wa kunukuu

Mie nadhani Mshahara unalemaza akili ile kila mwezi unasubiri kukinga mkono tena kwa kazi nyepesi nyepesi japo mwisho wake ukizeeka au kustaafu ndio KUBAYA, tofauti na kujiajiri mwanzo unakuwa mgumu sana ila ukitoka tuuuu ndio mazima.
 
Hivi mtu uliyeajiriwa kwenye ofisi ya mtu unaweza wekaa miguu kwenye meza, unaweza kuamua kuchelewa kazini. Muda wote unaogopa boss wako
Unamuongelea Boss wa aina gani..Hivi mfano kama umejiajiri kuuza samaki pale feri..utakuwa unaamka saa nane mchana kisa samaki ni wako nawewe ni boss?.....Au kama umefungua duka au dispensary, utakuwa unachelewa kazini kisa wewe ni boss...Au meneja wa consulting firm atakuwa analala hadi saa nne huku kuna project ya mtu (Kazi ya mteja) na haijaisha?....Mkuu...kila mtu ni Boss wa mwenzake ila tunatofautiana muda gani unakuwa na hiyo tittle....Unaweza kuwa Boss ofisini ila ukirudi home baba mwenye nyumba una mgwaya...trust me
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] utakuwa unafany kaz za watu wew sio buree[emoji23][emoji23]
 
Sasa kwanini hao walioajiriwa wakifukuzwa kazi au kustaafu wanaanza kuhaha kujiajiri tena, zile hela walizopata kule kwenye kuajiria hazitoshi au hizi za kuja kujiajiri ndio zitatosha.
Hivi hujaona watu ambao, walikua wafanyabiashara, biashara imeyumba na wenyewe wanayumba wako hoi.
 
Mkuu ww ni mwajiliwa bila shaka unatamani kujiajiri karibu upewe mbinu za kujiajiri. Kujiajiri ni raha sana
Unachotakiwa kujua maisha yanatofautiana, kuna watu wanafanya shughuri zao, wana shida sana, mfano, kuna watu wanauza miche ya bustani, kuna siku anatoka hana hela ya kula, huku mwajiriwa mwingine akiwa anatengeneza laki 5,000 kila siku ya kazi. Hivyo kama wewe umefanikiwa sehemu ulipo, Omba Mungu, uendelee kupata, lakini siyo kweli kazi yako inawazidi watu eote walioajiriwa.
 
Mkuuu nadhani upo sahihi kama unawaongelea walioajiriwa na kazini wana miaka zaidi ya minne na masilahi wanayo yapata ni kiduchu hayawafikishi kokote ni bora kujiajiri.Mm ni mmoja wapo ya wahanga ,mtu upo kazini unafanya kazi kweli kweli lakini hakuna anaekuona kama una msaada .Mtu unakaa kazini zaidi ya miaka 7 lakini unafanyia kula tu huna uwezo wa kusave.Tatizo tunakosa uthubutu lakini pia mazingira ya kujiajiri ni magumu but kama kungekuwepo urahisi wengi tungekuwa tushaachana na serikali toka kitambo.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Anzisha yako,weka paka wakufanyie kazi achana na watu wanakaa miaka mitano kufanya kazi.Weke hata madege ya angani yakusaidie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…