Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Nakwambia hivi, hata unaposema umejiajiri, bado umeajiriwa.Tofautisha Kati ya kuajiriwa na kujiajiri, vinginevyo rudia tena kusoma uzi,kina maeneo hujayaelewa.
Mathalani, anayesema amejiajiri kwa kunzisha biashara naye inambidi awe na good customer service kuwavutia wateja, hapo na yeye kaajiriwa na wateja anafanya kazi kuwavutia wateja.
Hilo moja.
Pia, ikiwa kila mtu atataka kujiajiri, hakuna atakayeweza kujiajiri.
Kwa sababu hao wanaojiajiri pia wanataka watu wa kuwaajiri, wanataka mifumo ya kiserikali ambayo ina watu walioajiriwa.
Kwa hiyo, ni ushamba na ufupi w amawazo kutaka kila mtu aajiriwe au kila mtu ajiajiri.
Sasa kuna mtu ndoto ya maisha yake yote ni kuwa Jenerali wa Jeshi la Tanzania.Ailinde nchi yake kwa kuwa mwanajeshi mwenye ushawishi mkubwa.
Sasa huyu naye unataka ajiajiri vipi wakati kuwa Jenerali wa Jeshi la Tanzania inabidi uwe muajiriwa wa serikali ya Tanzania kwa miaka mingi?
Unataka kusema watu wote wanaotaka kutumikia nchi yao kwa kuajiriwa serikalini hawana akili timamu?
Kwa nini unafanya unachotaka wewe ndiyo kiwe kitu cha akili timamu, na wanachotaka wengine si cha akili timamu?
Hao ma genius wakina Einstein walioajiriwa kufundisha vyuo vikuu na kufanya research wote hawakuwa na akili timamu?
Robert J Openheimer alivyoendesha Manhattan Project na kuvumbua bomu la atomiki alifanya kazi ya kuajiriwa na serikali, naye hakuwa na akili timamu?