Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.
Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?
Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.
Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.
Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?
Kwanini mnakaa kwenye ofisi za watu kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkistaafu au kutumbuliwa ndio mnaanza kukumbuka shuka la kujiajiri na huku muda wenu wote, nguvu yenu yote na akili yenu yote mmemalizia kwenye ofisi za watu.
Ina maana kazi zote za serikali afanye Raisi au vipi?
 
Unachotakiwa kujua maisha yanatofautiana, kuna watu wanafanya shughuri zao, wana shida sana, mfano, kuna watu wanauza miche ya bustani, kuna siku anatoka hana hela ya kula, huku mwajiriwa mwingine akiwa anatengeneza laki 5,000 kila siku ya kazi. Hivyo kama wewe umefanikiwa sehemu ulipo, Omba Mungu, uendelee kupata, lakini siyo kweli kazi yako inawazidi watu eote walioajiriwa.
Laki 5,000

100,000 x 5,000= 500,000,000/=

Ni kazi gani unapata 500,000,000 kwa siku ?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] utakuwa unafany kaz za watu wew sio buree[emoji23][emoji23]
Wewe tatizo lako hujavuka daraja la kujadili watu ukaweza kujadili hoja.

Hapo pa kujadili watu ndipo akili yako ilipoishia.

Hapa kuna hoja iliyo kubwa zaidi ya mtu yeyote mmoja.

Ila, hilo hujaliona.Umeona cha kujadili ni mimi. Mtu ambaye hata hunijui, hujui nina vitegauchumi gani, hujui natoka familia gani.

Na huwezi kujua kwamba inawezekana akawepo mtu mwenye biashara zake anafanya, na wakati huo huo anafanya "kazi za watu".

Yani akili yako imeishia kukariri kwamba lazima mtu awe anafanya "kazi za watu" au zake.

Hapo ndipo mwisho wa uwezo wako wa kufikiri.

Typical one track mindset ya wabongo wengi wasioweza kufikiri nje ya set parameters.
 
huna tofauti na wanasiasa wanaosema tujiajiri
Wakati wao wameajiriwa na serikali
 
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.

Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.

Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.

Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.

Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.

Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.
Anamaanisha mtu anaye work for money na anayefanya biashara yake make money
 
Anamaanisha mtu anaye work for money na anayefanya biashara yake make money
Hata biashara nayo ni "work for money", kwani kwenye biashara kuna hela inayokuja bila kufanya kazi?

Mimi nina nyumba ninapangisha, moja ya biashara rahisi kabisa.Lakini nayo mpangaji atataka umtimizie mambo fulani itabidi ufanye kazi kuweka nyumba sawa.

Hivi sasa nafungua kituo cha afya sehemu.Lakini hapo napo nafanya kazi na watu wa afya wa wilaya wanakagua, inabidi nifanye nao kazi kufikisha vigezo vinavyotakiwa ili niweze kuanzisha kituo cha afya.

Kwa hivyo hata kama nafungua sehemu biashara yangu, haina maana kwamba sitatakiwa kufanya biashara kwa kutakiwa kufikisha vigezo vya serikali, vya wateja, vya watu wengi sana.

Kwa hiyo habari ya mtu kufanya kazi yake ni uzushi ama njozi.

Watu wanategemeana, hakuna mwenye kufanya kazi yake mwenyewe.
 
Uwe umeajiriwa hapo unatafuta faida na ukijiajiri pia unatafuta faida haipo siku utafurahia maisha na mkumbuke kila kitu duniani ni biashara ya moja kwa moja au isiwe ya moja kwa moja yaani kila kitu mtu afanyacho analenga faida hivo kikubwa ni kukaa kibiashara
 
Mimi nawajua watu wana makampuni yao, wamejiajiri.

Wanafanya biashara ya kufuata "tender process", kupata biashara za serikali.

Wanawanyenyekea kichizi waajiriwa wa serikali wanaopitisha nani apate tenda na nani asipate tenda.

These things are not as simple as nani kaajiriwa na nani kajiajiri.
Tena huwa wana qualification sawa,hapo huwa tunaingia chemba tunaelewana.una kuta tenda ni ya 500M lazima awe mpole na mdogo kama piliton.
 
Tena huwa wana qualification sawa,hapo huwa tunaingia chemba tunaelewana.una kuta tenda ni ya 500M lazima awe mpole na mdogo kama piliton.
Wenyewe mnajua umaaluni mnaoufanya, wakiwakuta mmekalia viti vyenu mpaka shikamoo wanawapa vijana wadogo tu.

Halafu hasira zao wanakuja kuwamalizia hapa JF kisa mmeajiriwa.
 
Jamani haya mambo yanafundishwa toka form 1,specialization and division of labour.

Watu hufanya kazi tofauti tofauti kutokana na mazingira ya vitu vingi au mambo mengi,mwisho wa siku haijalishi unafanya kazi gani lazima utakuwa na Bosi katika kazi au shughuli yako.

Mifumo ya Duniani imewekwa kwa namna ambayo kila moja anawajibika kwa Mtu au kundi la watu,kwa namna hiyo kila Mtu ujira wake unategemea maamuzi ya Mtu au Watu.Kila Mtu ni mwajiriwa hapa Duniani.
 
Ukiona mtu anamjadili mwenzake badala ya hoja-za-mwenzake zake,
Ujue kuna tatizo.

Hoja mleta Uzi anashangaa inawezekanaje mtu kukubali kuajiriwa kwa miaka mitano,
Sasa tusiende nje ya mada tafadhali.
 
Kama natengeneza lets say tsh 100m per year kwa kutumwa na mwajiri ni wafanyabiashara wangapi wanatengeneza hiyo faida P.A kwa kutumwa na wateja wao?
 
Naona kuna notion kwamba kuajiriwa ni jambo baya, hili jambo nalipinga. Kuajiriwa bila maslahi yanayoridhisha ndiyo jambo baya. Hata CEOs wa Apple, Google, Microsoft, Alibaba, Toyota and the list goes on and on nao pia ni waajiriwa na wanakunja pesa ndefu kuliko mkaanga viazi wa Tandahimba aliyejiajiri.

Aidha kujiajiri/ujasiliamali ni kuwa muajiriwa wa wateja wako. Wateja wako ndio mabosi wako. Utatenda vile watakavyo na kucheza mziki wao. Kifupi kukimbia kuajiriwa ni kuacha shughuli zote na kulala tu nyumbani.

Wewe unayepinga kuajiriwa siku ukianza ujasiliamali wako utahitaji hao hao waajiriwa. Kila mtu akiwa na mawazo kama yako sijui mtatoa wapi nguvu kazi.

Cha msingi ni kulipa watumishi maslahi stahiki.
Yah nakubaliana na wewe, kuajiriwa sio tatizo ila tatizo ni kuajiriwa sehemu isio na maslahi sehemu ambayo hukui kimaisha unakuwa kama mtumwa tu miaka nenda rudi!
 
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.

Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.

Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.

Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.

Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.

Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.
"Tafsir nyepes za juu juu".
Hili ndio tatizo kubwa..
 
Unakuta mtu anapokea mshahara wa milion 4 , halafu mke wake Yuko mkoa mwingine abafanya kazi ya mshahara wa laki 9. Halafu familia Yao inaishi na house girl.

Unawauliza hivi mnashindwa kujiajiri mkae na familia. Wanajibu kazi kwanza. Huwa nashangaa Sana mentality za namna hii.
Hahahah kazi kwanza au sio? Huyo mwanamke wa kukaa mkoani labda awe amenioa mimi! Vinginevyo ni kumuweka dukani tu hapa hapa mjini apambane na wateja
 
Back
Top Bottom