Kwanini niwaache? Kwanini mtu mzima mwenye miaka 50 anasumbuliwa na Mapenzi? Kwamba hajawahi kuona nini kwenye maisha yake?
Ngoja nikuelezee kwa mjibu wa kisaikolojia,ni kwamba ubongo wa binadamu unaakili nne,,moja inapatikana darasani ili kuitambua,ambayo ni IQ ,,nyingine tatu hazipatikani darasani,bali yategemea nani kakulea, plus mazingira uliyokulia na hasa kuchangamana na watu wengine.
Hivyo kwa kifupi hao jamaa zako,wamekosa hizo akili tatu,,mtu kama katika maisha yake akuchangamana na hata marafiki wenzake hata utotoni na ukubwani,katika michezo mbalimbali uko ndiko uibuka vipaji,ubunifu nk nk,,anaweza akawa injinia mzuri,lkn akikosa hizo akili tatu,atafeli katika maisha,kwakuwa kabaki tu na ego ya usomi wake,hana mbinu za kukabiliana na changamoto za ndoa yake,kwa kuwa hana uzoefu tangia huko nyuma.
Hivyo kwa ushauri wangu waacheni watoto wenu wacheze na wenzao,msiwafungie,kuna mengi wajifunza kupitia kucheza,bila kusahau kwenda ibadani,pia mfanye mwanao atambue kua kuna kukosa, pengine mzoeshe anywe ata chai isiyo na sukari,usimzoeshe kupanda gari mara kwa mara,sehemu anayoweza kutembea hata kwa miguu,mpitishe katika maisha yenye changamoto,ili aelewe kuwa kuna changamoto katika maisha,.atakapojitegemea changamoto yoyote ikimkuta itakua rahisi kuikabili.,🙏🙏🙏💪💪