Kuna haja, ni muhimu kubadilisha maji angalau mara moja kwa mwezi ili usibadilishe maji inakupasa kuwa na best mechanism ya maintain water quality kwa kutumia vifaa maalumu vya kuongeza hewa kwenye maji (Aerators) na kifaa maalumu cha kuchuja maji (bio filter)
Kitu kinachofanya kuwe na urazima wa kubadilisha maji kila baada ya muda fulani uwa ni kudhibiti ammonia level, ambayo inatokana na kinyesi cha samaki na mabaki ya chakula (uneaten feed), ammonia ikizidi kwenye maji uwa ni sumu kwa samaki hivyo inatakiwa kudhibitiwa either kwa kubadilisha maji au kuchuja maji kwa kutumia bio media.
Tumia pond liner kama hizi kupunguza gharama za ujenzi lakini kama uko vizuri financial basi jenga bwawa (Concrete pond). Utakuwa ukivuta maji toka kwenye kisima kwa kutumia pump na kujaza bwawa lako.
Ahsante sana ngoja nifanye tathmini