Hivi Jehanamu iliumbwa lini?

Jehanam/Kuzimu ni mahali pa mateso hapo awali palipotayarishwa na Mungu kwa ajili ya shetani na malaika zake (Mathayo 18:9; 25:41). Maneno Hadesi (Kigiriki) na Sheoli (Kiebrania) nyakati fulani huhusishwa na kuzimu. Hata hivyo, Hades/Sheoli ni mahali au ulimwengu ambapo roho za watu huenda wanapokufa (ona Mwanzo 37:35). Hadesi/Sheoli si lazima mahali pa mateso kwa sababu watu wa Mungu walisemekana kwenda huko pamoja na waovu. Katika Agano Jipya, tunaona kwamba Hadesi kwa namna fulani β€œimegawanywa.” Hiyo ni, ulimwengu wa wafu umegawanywa katika mahali pa faraja na mahali pa mateso (Luka 16:19–31). Kuna maneno mengine yanayohusiana na kuzimu katika Biblia kama vile Gehena na ziwa la moto. Ni wazi kwamba kuna mahali halisi ambapo roho za wasiookolewa huenda milele (Ufunuo 9:1; 20:15; Mathayo 23:33). Kila kitu kilichowahi kuwako au kilichopo au kitakachokuwa kimeumbwa na Mungu, pamoja na kuzimu (Wakolosai 1:16). Yohana 1:3 inasema, β€œVyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kumtupa mtu motoni (Luka 12:5). Yesu anazo funguo za mauti na kuzimu (Ufunuo 1:18). Yesu alisema kwamba kuzimu β€œimetayarishwa” kwa ajili ya Shetani na roho waovu (Mathayo 25:41). Ni adhabu ya haki kwa mwovu. Jehanamu, au ziwa la moto, itakuwa pia mwisho wa wale wanaomkataa Kristo (2 Petro 2:4–9). Habari njema ni kwamba watu wanaweza kuepuka kuzimu. Mungu, katika rehema na upendo wake usio na kipimo, amefanya njia ya wokovu kwa kila mtu anayemwamini Mwana wa Mungu, Yesu Kristo (Yohana 3:16, 36; 5:24).
 
Ipo lkn huwezi jua kama ipo kama huna elimu kuhusu ulimwengu usioonekana
Lakini Mbingu nayo Ni sehemu isiyoonekana Ila iliumbwa,na iwe Mbingu ikawa!Sasa mbona sijasoma na iwe iwe Jehanamu ikawa!
 
Moto ukawa mweusi.

Ina mana hapa hata ile ROYGBIV hai apply?? Moto uwe mweusi???

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Nimevisoma vifungu vyote,na sijapinga uwepo wake,Ila msingi wa Swali langu Ni lini iliuumbwa?mbona vitu vyote vikubwa vimeelezewa uumbaji wake kwanini uumbaji wa Jehanamu umesahaulika?Kuna haja ya kuupdate maandiko ?
 
Nahisi hiyo siku ikifika Mungu atatengeneza shimo kubwa atalitumbukiza Jua humo shimoni pamoja na watu ili liwachome
 
Nawe ukaamin ipo😁
Tangia ninaanza Sunday school Nina miaka mitano naambiwa nikitenda dhambi nitaenda huko Hadi Sasa na Mimi naambia hivyo watoto wangu nitaachaje kuamini sasa!?SEMA ndio inafikirisha sasa
 
Nahisi hiyo siku ikifika Mungu atatengeneza shimo kubwa atalitumbukiza Jua humo shimoni pamoja na watu ili liwachome
Halafu umewaza kitu!Bora wangetuambia Jehanamu Ni kwenye jua ingekuwa poa Sana.
 
Ni kweli, MUNGU NI PENDO...ukute ndio maana Hakuna sehemu kwenye uumbaji umeonyesha aliumba hiyo kitu
 
Ila imezaa matunda, saiv raia ziko kwny mstar everythng ni yes
Na nidhamu ya uoga juu, raia hatutaki hata kujiuliza maswali yanayotutatiza Ni kuogopa kwa kwenda mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…