Hivi kati ya chatgpt, Gemin na meta AI nani anatoa taarifa za kweli?

Hivi kati ya chatgpt, Gemin na meta AI nani anatoa taarifa za kweli?

Claude kwangu ndo namba moja.Cha muhimu ujue wote hao hakuna aliye 100% correct, kuna siku ChatGPT kanambia Papa Francis yupo hai wakati ashazikwa. Nikajiuliza je ambavyo sijui si huwa ananidanganya sana? Hata huyo Claude ashawahi kunilisha matango pori.
 
Chat Gpt yuko kote yaan formal na informal utakavyompeleka ndo ataenda ana vibe utani mwingi n.k

🤣 Gemin imekaa kifaza sana ! Yaan kama mtu yule ambaye hapendi kona kona amenyooka ! Hajui utani imekaa kama baba mkwe !!

Kuna siku nimemuuliza ChatGpt "Oya nna 500k kwa hela ya madafu hapa mshua hivi siwezi pata Maserati" akanijibu "kwa hiyo pesa huwezi kununua hata tairi yake ila unaweza kununua picha yake ukabandika ukutani au Toy ya maserati ukampa mtoto" 🤣

Juzi nimemuuliza kama anaweza recommend acid inayoweza kudissolve kuku wa uzito wa kg 80 🤣🤣
Lakini ukae ukijua jinsi unavyozidi kuiuliza mambo kiutani ndivyo nayo inaendelea kukufahamu wewe kihivyo
 
Gemini. Hao ni Google mkuu, wako connected karibia na websites zote Duniani ikiwemo hii, Taarifa zao zipo updated muda wote. Sema tu hawana lugha ya kihuni kama Chat GPT, ila siku zijazo ukweli utajulikana.
Fact. Wamenyooka lugha ngumu na utan kwao hamna
 
Kama una uwezo wa kulipa lipia claude. Ndiyo maana inaongoza kwa kutengeneza faida... Wana models ambazo ziko optimized kwa special tasks
 
Tatizo deep seek wanatumia chainizi
Screenshot_20260811_173941_DeepSeek.jpg
 
Mi nampenda ChatGPT ingawa sometimes anaweza akawa na jibu la direct lakini still akakuzungusha na maelezo mengi, atakupa jibu mpaka umbane sana...

Kuna kipindi niliamua nimuulize ChatGPT "Kati ya Ronaldo na Messi nani ni Mchezaji bora zaidi yaani GOAT?"

Akajibu, "Huo ni mjadala mpana sana, Messi na Ronaldo wote wawili ni wachezaji bora... Kulingana na takwimu zao, maoni ya mashabiki, makocha, wachezaji na wadau wengine ni ngumu kusema nani ni bora zaidi... Messi ana kipaji asilia, na pia ni playmaker mzuri.. Ronaldo yeye ni Mchezaji mwenyewe nguvu, kasi na pia ni mwanamichezo zaidi.. Kwa hiyo ni ngumu mimi ni ngumu kukuambia yupi ni bora"

Nikamkazania, "hebu niambie yupi ni bora kwa mtazamo wako?" Akajibu "Ni ngumu kusema yupi ni bora, wote wawili ni bora"

Nikamwambia "Sitaki uniambie wote ni bora, mimi nataka uniambie mmoja ambae ni bora zaidi"... akajibu "Ukiangalia takwimu na maoni ya wengi Messi ni bora zaidi"
 
Back
Top Bottom