Hivi kati ya mwanamke na mwanaume nani anatakiwa kubadili dini ili aoe au kuolewa? Na kwanini?

Hivi kati ya mwanamke na mwanaume nani anatakiwa kubadili dini ili aoe au kuolewa? Na kwanini?

Tafuta wa dini yako mkuu,

Mwanaume unabadilisha vipi dini kisa mwanamke?? kama dini utabadili ukamfuata jiandae kuumia zaidi mana ashakuona huna kauli juu yake wala maamuzi yake

Kiutamaduni mke hufuata mume, mume humtoa binti kwao na kwenda kuishi naye sio mke anamtoa mume kwao ingekua hivo msingekua mnakuja majumbani kwa wanawake mnaotaka kuwaoa kutaka idhini
 
Vyovyote itakavyokuwa ni undezi kiwango cha lami kwa mwanaume kubadili dini sababu ya mwanamke.

Ukibadili dini sababu ya mwanamke inamaanisha unaweza hata badili jinsia yako sababu ya mapenzi.

Mwisho wa siku mnaoana ni nyinyi wawili na si imani zenu.
 
Sio lazima kubadili dini mkipendana kwa dhati inatosha kila mtu ataabudu anakokujua
 
Naombeni mnisaidie kuna mdada nimempenda anakata kubadili dini anasema nibadili mimi .
Mwanamke Hana Dini, Sijui ulifundwa wapi wewe jambo jepesi kama hili unashindwa kuling'amua.
Sasa huko kwenye ndoa si ndo utakuwa unalia kila siku maana huko ndo kugumu zaidi.
 
Ni hiyari ya mtu na makubaliano yenu, yoyote anabadili.

Ila kubadili dini kwa ajili ya mtu mmh, dhehebu tu siwezi badili.
Unafiki wa dini siwezi
Tutapendana na kuishi vizuri ila kila mtu abaki na dini yake.
 
Kitendo cha kuja kuomba ushauri inamaanisha tayari ushakata shauri lako, unachotaka hapa ni validation ya maamuzi yako tu.

Ila kumbuka mwanaume kila ulichonacho kuanzia jina mpaka dini yako huo ndio utambulisho wa uanaume wako. Kubadili chochote kati ya hivyo basi ushabadili nafasi yako ya uanaume.

Jiulize kwanini mwanamke huchukua jina la mume akiolewa na si la mke?? Inamaanisha mwanaume ndie wa kufuata kwa kila kitu.

Huyo mwanamke keshajua wewe ni dhaifu kwake, hakufai. Baada ya dini atakwambia ubadili kabila pia kumaanisha ukane asili yako.
 
Back
Top Bottom