Hivi kati ya mwanamke na mwanaume nani anatakiwa kubadili dini ili aoe au kuolewa? Na kwanini?

Hivi kati ya mwanamke na mwanaume nani anatakiwa kubadili dini ili aoe au kuolewa? Na kwanini?

Utafiti unaonesha wote waliobali dini kwa sababu ya wanawake kwenye ndoa zao wanaburuzwa na wanaishi kwa mateso[emoji1]
 
Ni mwiko mwanaume kuhama asili yake kidini, kabila, ukoo, uzawa, jina sababu ya mwanamke, mi kwanza mwanaumr akishakubali kunifuata kimojawapo kati ya hivyo namuacha papo hapo, hafai ni kopo la kiume sio mwanaume huyo
 
  • Kicheko
Reactions: Avs
Mwanaume unabadilishaje dini mzee
Nishapiga sana chini wanawake kwaajili ya dini tena wanawake wa maana kweli kweli ila kwangu ukija kwenye ishu ya dini huwa sina masihara unanifata twende huwezi pita kushoto navuta nyingine No discussion
 
Acha kumuendekeza huyoo, yafaa mwanamke kutii wew ndio mtoa maamuzi.
 
Naombeni mnisaidie kuna mdada nimempenda anakata kubadili dini anasema nibadili mimi .

Hapa ndipo watu wengi wanapokosea

1. Usije ukabadili dini kwa sababu ya ndoa badili dini kwa sababu umeifuatilia kiundani na umeridhishwa na dini hiyo ,hata ikatokea mtu akakuuliza maswali unaweza kumjibu kwa kujiamini kabisa maana unaielewa vizuri dini husika.

2. Ukiona mtu anabadili dini kwa sababu ya ndoa jua kwanza hana msimamo kingine ni mwepesi sana kushawishika /kudanganyika.

3. Kuwa jinsia fulani haikufanyi wewe kuwa ndiyo wa kufuata upepo suala la imani ni suala zito mno ,na wengi wanaofuata upepo huwa wanarejea kwenye dini zao hapo ndipo familia inaanza kuingia misuko suko.
 
Mahitaji yataamua nani abadili. Yaani mwenye uhitaji hatasita kukubali kubadili dini kwa namna yoyote ile.
Sometimes yanakuwa ni makubaliano ya wawili tu bila kumshirikisha mtu. Wengine hufanya makubaliano baada ya kupata baraka za wazazi wao. Hii ni nzuri zaidi.
 
Du ukishabadilisha dini atakuambia uende Jim ukatafute six pack.
Hicho ndyo kipimo Cha kwanza mwanamke huyo anakifanya kuona msimamo wako.Tumia fursa vizuri.

Ukicheza vibaya atakuja kukuambia kwanini usioshe vyombo wewe Mimi nimechoka.
 
Kama hataki kufuata dini yako basi kila mtu abaki na dini yake.
 
Back
Top Bottom