Hivi kile kizazi cha watumwa waliokuwa wanachukuliwa na waarabu kutoka Tanganyika kiliishia katika taifa/mataifa yapi?

Mkuu hukupiga nao picha?
 
Mkuu hukupiga nao picha?
Mkuu sio yeyote unakutana nae duniani unampiga picha besides walikuwa sio watu wa karibu ila angesema kuwa asili yake ni mnyamwezi mbona ningefunga undungu 😄

Ila wapo wengi huko ila picha sina
 
Asante sana Mkuu, watumwa wanavibweka sana
 
Waarabu na majahazi yao yalichukua watu wachache tofauti na meli kubwa za wazungu.
Nenda Saudia,Oman hadi India watu weusi wengi sana wamekuwa assimilated na wengine machotara, ukisoma historia ya Iraq ya enzi hizo Kuna miaka mia tatu ilitawaliwa na vizazi vya watumwa toka Afrika Mashariki.
Mwisho waliopelekwa nchi za Marekani waliopelekwa na wanawake wazaliane na kupatika watumwa wapya wa bure.
 
Afadhali hata wamarekani tunawaona waafrika huko ila hawa waarabu sijui waliwapeleka wapi waafrika, maana hatuwaoni katika mataifa yao, tuone hata machotara tu
Uarabuni ni jangwa hakuna mashamba, mashamba yalikua America na ulaya. Waarabu walikua wanafanya biashara ya watumwa ,kuwauzia wazungu ili wapelekwe mashamban huko amerika
 
Hilo jina Jesus lisikuchanganye sana, kwa Wareno ni jina la kawaida kabisa. Kuna Jesus mwingine anacheza Arsenal. OKORU NO O YAMERU
 
Nitafutie Dili la kazi za Ujenzi uarabuni.
 
ni jamii hiyohiyo ya waarabu, sijui kwa nini huwa mnawatoa wairan kwa waarabu wakati ni jamii moja na wamo katika jumuiya ya nchi za kiarabu

Waarabu ni watu wanaoongea Kiarabu kama lugha yao ya kwanza. Wa Iran wanaongea Farsi kama lugha yao ya kwanza, hawaongei Kiarabu kama lugha yao ya kwanza.

"Iran and Turkey are not Arab countries and their primary languages are Farsi and Turkish respectively. "

 
Umeongea ukweli usiopingika
Nashangaa mijadala kama hii inakuwa ya kutetea upande badala ya kusema yaliojiri
Walichofanya hao kwetu ni Jambo baya sana na walitakiwa hata walipe ushenzi huo
Ila mada ilikuwa tofauti ikarudi kwa baadhi kuanza kejeli na matusi

Hivi kweli waarabu wawabebe maelfu wawapeleke kwao hata maendeleo hakuna na ardhi ya kulima hakuna
Sasa wakafanye nini huko
Wakati wao pia njaa
Wazungu waliwachukua kwenda kuwalimisha mashamba
 
Watu watembeemiji kama Tabora, kigoma , lindi ambapo waarabu waliishi wapi na walipokuja wazungu walikaa wapi, utagundua mwarabu alichanganyika na mzungu alijitenga kama kusoma huwezi basi tembea na fikilia
 
Afadhali hata wamarekani tunawaona waafrika huko ila hawa waarabu sijui waliwapeleka wapi waafrika, maana hatuwaoni katika mataifa yao, tuone hata machotara tu
Acha upuuzi wewe asilimia kubwa mwarabu alikua anamuuzia mzungu watumwa na hata hivyo mbona waarabu weusi wapo wengi tu
 

Hawakuwachukuwa tu waliwanunua kwa pesa , Hata machifu wa kiafrika waliwauza kwa kupata pesa
 
Kwani uliwahi kuona mwarabu anaolewa na mweusi? Tafuta kama utapata. Wengi walihasiwa kwa hiyo hawakuzaliana. Wengi wanaoonekana ni kizazi Cha wanawake waliobakwa na ndio maana hawana majina ya kiafrika au hulka ya kiafrika. Wamerithishwa utamaduni wa kiarabu na baba zao, na wengine wametengwa.
Hata Leo waafrika wanaonenda Uarabuni kutafuta kazi hawapewi uria bali wanapewa Kibali Cha kuishi na kufanya kazi tu.
 
Acha upuuzi wewe asilimia kubwa mwarabu alikua anamuuzia mzungu watumwa na hata hivyo mbona waarabu weusi wapo wengi tu
Watumwa waliosafirishwa kwa njia ya Zanzibar wengi walienda bara Hindi na Uarabuni kwenyewe. Walienda kwa wazungu walipelekwa visiwa vya Reunion, Mauritius n Madagascar. Bado tunawaona.
Kuna matanga yalikua yanafanya safari kwenda Uarabuni mengi tu na hakuna kizazi hicho. Mpende Mungu na kumuabudu Mungu. Ruhusu mwarabu akosolewe.
 
Mwarabu aliwaminya kende hao masalia mnaowaona wametokana na wanawake waliobakwa
 
Mbona nchi za wazungu weusi wako huru sana? Tunawaona kwenye mpira, muziki na shughuli zingine.
Barack Obama, 50 Cent, lil wayne, movies km zote nk. Ufaransa ndiyo wapo wengi sana.
Waarabu kutoka Syria walikuwa wanakufa majini wakienda nchi za ulaya
Kuwaona hao wa USA sawa unawaona jee lakini unaijua system yao walio wekewa kuishi huko?.

Angalia level ya elimu yao na maisha yao wanavyo ishi ukienda USA hao black wakipata hela wanahama kwenye neighborhood zao(PJ). Na kuhamia neighborhood za white na huko kwa white nako hawapewi heshima kama ya ukaazi kama ya white. Watu weusi wanahitaji kujitukuza kuanzia barani kwetu Afrika ili kwengine tupate heshima pia.

Lakini leo tourists ana thamani kuliko mzaliwa kipaombele cha utalii kipo mbele zaidi kuliko kipaombele cha wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…