Hivi kulingana na biblia nani alikuwa ni nabii wa mwisho na nani alikuwa ni mitume wa mwisho ?

...nabii huyu alikuja na kitabu kingine cha quran chenye asilimia 90 ya maneno ya kwenye biblia ikiwemo, habari za adamu na hawa, ibrahimu, isaka, yakobo, musa, na hata habari za yesu zilizopo kwenye quran alikuja nazo
Ni lazima maandiko yafanane kwa sababu waanzilishi halisi wa hiyo dini yake ni WAKATOLIKI, yeye walimtuma kutekeleza tu..
 
sikiliza cha muhimu utubu kwani hili ndio jambo la msingi kweli kweli linalobeba hatima yako tubu basi kabla muda wako haujaisha
 
Weka andiko
nitajie list ya manabii unao wajua kwenye biblia kwa mtiririko wa vizazi vyao je wamwisho ni nani nitajie jina lake ? je, siyo huyu wa ufunuo ambaye ni yohana ?
 
nitajie list ya manabii unao wajua kwenye biblia kwa mtiririko wa vizazi vyao je wamwisho ni nani nitajie jina lake ? je, siyo huyu wa ufunuo ambaye ni yohana ?
Karama ya unabii imetolewa bure kwa yeyote. 1 wakorintho 13.
Hata wewe ukitaka unakuwa Mungu akiridhia.
Ukisema hakuna nabii unasema hakuna roho mtakatifu, au hakuna karama za roho
 
Karama ya unabii imetolewa bure kwa yeyote. 1 wakorintho 13.
Hata wewe ukitaka unakuwa Mungu akiridhia.
Ukisema hakuna nabii unasema hakuna roho mtakatifu, au hakuna karama za roho
manabii huwa wanasimama kwaajili ya nini ?
 
Karama ya unabii imetolewa bure kwa yeyote. 1 wakorintho 13.
Hata wewe ukitaka unakuwa Mungu akiridhia.
Ukisema hakuna nabii unasema hakuna roho mtakatifu, au hakuna karama za roho
wewe unamfahamu roho mtakatifu kama nani ?
 
Karama ya unabii imetolewa bure kwa yeyote. 1 wakorintho 13.
Hata wewe ukitaka unakuwa Mungu akiridhia.
Ukisema hakuna nabii unasema hakuna roho mtakatifu, au hakuna karama za roho
karama za roho ni zipi ?
 
nitajie list ya manabii unao wajua kwenye biblia kwa mtiririko wa vizazi vyao je wamwisho ni nani nitajie jina lake ? je, siyo huyu wa ufunuo ambaye ni yohana ?
Huu msumari dizaini kama ulikuwa special sana kwa Apostle kuna muujiza (kawe 1 hiyo). Sema nini usichanganye mambo kumbuka kuna Yohana mbatizaji ndiye aliyeandaa njia ya kumpokea masihi ndiye tunaweza tukasema nabii wa mwisho.

Yohana aliyeandika kitabu cha ufunuo akiwa kisawani patmo alikuwa ni miongoni mwa mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo.

All in all mtawatambua kwa matendo yao.

Kuna verse hadi imesema kuna atakaye shusha hata moto toka juu na masela kibao watajua ndo Mkuu wa kazi kumbe ujio wake yeye hautii shaka kila mtu ataona na atakiri....
 
Sijasoma bandicoot lako lakini swali ulilouliza lina jibu lake. Hakuna Mtume au Nabii wa kwanza wala wa mwisho. Mungu amekuwa akifanya kazi duniani tangu amuumbe Adam. Kikubwa ni utambue kwamba katika Agano la kale kulikuwa na mgawanyo wa aina tatu wa watumishi wa Mungu.
1. Nabii
2. Kuhani
3. Mfalme.
Yesu Kristo alipokuja duniani yeye ndiye alihitimisha Agano la kale na akaanzisha Agano Jipya kupitia Damu yake msalabani. Baada ya kufufuka ndipo akawafanya wanafunzi wake kuwa Mitume. Kisha kupitia mitume hao Mungu akaanzisha kanisa. Na kupitia kanisa akaweka huduma 5 ambazo ni:
1. Mitume
2. Manabii
3. Walimu
4. Wainjilisti
5. Wachungaji.
Huduma hizo zitaebdelea kuwepo hadi Yesu Kristo atakaporudi duniani. Hivyo hakuna Mtume wala Nabii wa mwisho. Lakini pia wakati Yesu akikaribia kabisa kurudi kutaibuka Nabii Mkuu wa uwongo na Kristo wa uwongo. Yesu atakuja kuwakamata yeye mwenyewe na kuwatupa Jehanamu live kwa mujibu wa kitabu cha Ufunuo
 
manabii huwa wanasimama kwaajili ya nini ?
matunduizi
naomba nikusaidie manabii walisimama kwa ajili ya kazi moja na kabila moja na taifa moja kwaajili ya kuwasilisha neno la mungu ambalo kwa sasa ni biblia je hii biblia imekamirika hebu nijibu hapa hivi hii biblia imekamilika au haija kamilika ?

kama jubu lako likiwa imekamilika
ni vitu gani vinaweza kuonesha kuwa biblia imekamilika kikamilifu ?

maana hoja yako ipo kwenye jinsi manabii wanavyo patikana na sio yupi ni wa uongo na yupi ni wa kweli umesema vyema mungu ndio alie chagua nabii tangu zamani sasa hapa kipengele kipo kwenye yupi wa kweli na yupi wa uongo, ili kurahisisha hapa itabidi tutumie biblia yenyewe iongee ioneshe kuwa yupi ni nabii kwa hakika kila kilicho nje ya biblia ni cha uongo na kila kilicho ndani yake ndio cha kweli japo hoja yako ipo kwengine kwenye jinsi manabii wanavyotokea unaweza kuona kisa cha musa jinsi mungu alivyo mfanya musa kuwa nabii alafu linganisha na fungu lako hapo
 
hivi umesoma kisa cha yesu au hata kutizama filamu yake nzima ukamshuhudia yesu au mtume akiunda kanisa ?
 
Dah, nd
Ndefu mno halafu umechanganya mambo.
Sijakuelewa uliposema manabii wote hawakuanzisha kanisa, ina mana hata Yesu mwenyewe hakuwa na Kanisa?
Yesu aliabudia wapi kama hakuanzisha kanisa!
 
Dah, nd

Ndefu mno halafu umechanganya mambo.
Sijakuelewa uliposema manabii wote hawakuanzisha kanisa, ina mana hata Yesu mwenyewe hakuwa na Kanisa?
Yesu aliabudia wapi kama hakuanzisha kanisa!
yesu hakuanzisha kanisa lolote hebu kasome kisa cha yesu chote utaona hata wakati wa kuomba yesu alipiga magoti kwenye jiwe na kuomba yesu alienda kwenye vikundi vikundi na kuhubiri na kufundisha watu na sio aliunda kanisa yesu hakuwai kuunda kanisa hebu soma maandiko upate maarifa
 
Mkuu sijasoma lakini naahidi nitarudi kusoma Kwa Uzuri na jug la juice pembeni.

Kwa utangulizi tu nabii wa mwisho alikuwa Yohana mbatizaji.
 
Unapokosoa watu na huduma zao za kiimani uje na hoja za kimaandiko, sio hisia zako binafsi. Na uandishi wako una makosa pia mfano;
Yohana aliyeandika kitabu cha Ufunuo sio nabii ni Mtume, nabii wa mwisho wa agano la kale ni Yohana Mbatizaji hawa ni watu wawili tofauti.

Umewaita manabii, watu kama Yusufu, Eli, Henoko watu ambao hawakuwa manabii. Hili ni kosa ambalo linakuondolea credibility ya kuwakosoa hao manabii uliowataja hasa pale unapojihesabu kama msomaji wa Biblia

Halafu unasema manabii hawakuwahi kufungua makanisa na walikuwa waIsraeli, ni wapi Mungu alisema manabii watakuwa waisraeli tu? Una reconcile vipi na andiko kama la WAEFESO 4:11 ?

Ni kweli kuna shida siku za leo, wanaojiita manabii wengi hawafanyi ambacho manabii wanatakiwa/walitakiwa kufanya lakini hata wakosoaji nao hawajui namna ya kukosoa kwa hoja za kimaandiko ukiwemo wewe mleta mada
 
asante sana
 
Huna akili,umeandika utumbo mreefuuuu
 
Hii vita ya wakweli na waongo haina mwisho maana kila mtu ana hoja zake timilifu za kujitetea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…