Hivi kumbe kuna watu wanafanya biashara Dar es salaam kwa mtaji wa elfu 50 tu🙌🙌

Hivi kumbe kuna watu wanafanya biashara Dar es salaam kwa mtaji wa elfu 50 tu🙌🙌

50 nyingi hivyo,watu wanamitaji chini ya 50 na wanaishi,Biashara shida sio mtaji Biashara inahitaji wateja

ukishakua na wateja hata mtaji wa maneno tu,unaishi..kuna watu nawajua kila siku anaenda k.koo (sio kwenda kubeba mzigo) bali kwenda kuuza bidhaa kwa maneno.

unamkuta kasimama nnje ya duka kama Jinga,mteja ukiulizia kitu mwenye duka akisema Hamna yeye anamkosoa mwenye duka anamwambia "wewee si vipo stooo" Mteja unaambiwa kaa subiri nikuleteee..

Jamaa anaua winga kukufatia bidhaa unayotaka kwenye machimbo yake,anakuletea anakupiga "BEI ELEKEZI'' Ukitoa hela anakata chake unasepa,faida anatia mfukoni..Anasubiri mteja mwingine.

Kwa siku akirudi na hela ndogo kabisa ni 30,000... (mtaji wake ni mdomo tu)
 
50,000

Nunua box za protector sh 4000 kila Box inakaa protector 10 nunua box 10 tu = 40,000 bakisha 10 Lako la nauli toka area 1 to area 2

unapoint protector zinazoingiliana na simu nyingi, Box 1 (smart 4) Box 2 (hot 10i)nk

mabox 10,zungusha mguu kwa mguu kwenye BAR na PUB na migahawa,achana na faida nyingi uza Protector 1 kwa 3000 tu, Usipolaza faida

ya 10,000 to 20,000 kwa siku na hapo umeshakula njoo nitukane mimi na wote wa damu yangu.
 
Mmh biashara gani tujuze
Kama unaishi kwenu kuna blenda na friji, kanununue matunda ya elfu 30 sokoni na sukari ya 2500, saga juisi ipoze kwa ubaridi wa kutosha nununua glass za take away na milija yake elfu 7 kauze mtaani, obviously day one itakua ngumu but nakuhakikishia after a week utakua unapiga mpunga mpaka elfu 30 faida tu
 
Hamna biashara inalipa kwasasa kama biashara ya delivery,biashara n nyingi

lakini ukitaka fanikiwa chap chap mtu unamtaji wa chini ya 50,000 ni lazima ubuni

biashara ambayo utamfata mteja hadi mlangoni alipo,hizi biashara za kusema sijui

uchome mahindi,sijui ukaange mandazi kila mtu anafanya kama ukiamua zifanya

hizo biashara kachomeee hayo maindi na hayo mandazi hadi walipo wateja (jambo ambalo n gumu)

saivi ni kuwaza biashara ya kupga mguu kwa mguu yani mteja unafatwa hadi ulipo,Je swali?

Biashara Gani Hizooo? waza wazua biashara zipoo ila ondoa wazo la kukaa sehemu 1, 50k dar nyingi sana.
 
Kwa kweli kuna watu wanajua kubalans maisha ya Dar. Mtu ana mtaji wa elfu 50 anaingiza faida ya elfu 15 mpaka 20 na anaishi Dar vizuri tu.

Nawashangaa sana Wasomi wengi wakipewa milioni 1 wanadai haitoshi wanaishia kuidumbukiza kwenye starehe

“Nawashangaa sana wasomi”. Si kila mtu anaweza kufanya biashara.
Wengine lazima waende kwenye sekta zingine
 
Kwa kweli kuna watu wanajua kubalans maisha ya Dar. Mtu ana mtaji wa elfu 50 anaingiza faida ya elfu 15 mpaka 20 na anaishi Dar vizuri tu.

Nawashangaa sana Wasomi wengi wakipewa milioni 1 wanadai haitoshi wanaishia kuidumbukiza kwenye starehe
Sio starehe sema kubeti😅😅
 
Back
Top Bottom