Mkuu, ujanja ujanja unaanzia hapo kwenye kutengeneza list ya betting. Wanacheza na saikolojia.
Unakuta mtu ana furaha kashinda elfu hamsini, unamuuliza how? Anasema mkeka umetiki, unamuuliza ulibet kiasi gani, anajibu 40,000/= ukapata kiasi gani, anajibu 50,000/= sasa umeshindaje 50,000/=? Umeshinda 10,000/= hii 40,000/= ni ya kwako.
Makampuni yanakupa hongera kwa kukurudishia pesa yako kama ushindi. Hawatenganishi ushindi halisi ulioupata na pesa uliyoweka. Wanaharibu tafsiri ya ushindi kwenye ubongo wako.