Ili Gaza imalizwe ipo wazi jeshi la anga limeshindwa, IDF ina deploy na kuongeza askari ardhini kitu ambacho Hamas wapo vizuri zaidi kuliko IDF... hivyo niseme IDF ni overrated...
Kingine Israel ilikuwa inafanya standoff bombing pale Iran, kama wanashambulia Dar, wataishia Morogoro na kuachia smart bombs kusafiri hadi Dar, maana Iran bado ADs zilizobaki zilikuwa zinalinda anga... not true waliteka anga la Iran..
Labda tu mimi nikueleze vita si ku-edit picha au video au post za JF.
Katika jeshi lolote la kitaifa, muundo na idadi ya vikosi vinavyohitajika hutegemea mambo kadhaa, kama vile ukubwa wa nchi, malengo ya ulinzi, bajeti, na mkakati wa kijeshi. Hata hivyo, kwa kawaida, jeshi linahitaji vikosi mbalimbali vinavyofanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi. Vikosi hivi vinaweza kugawanywa katika kategoria za msingi kama ifuatavyo:
1.
Jeshi la Nchi Kavu (Army):
- Hili ni kikosi cha msingi kinachohusika na ulinzi wa eneo la nchi kwa njia ya vita vya ardhini.
- Vinasimamia ulinzi wa mipaka, operesheni za kijeshi ardhini, na kusaidia wakati wa majanga ya kitaifa.
- Mfano wa vitengo: askari wa miguu, vikosi vya magari ya kivita, silaha za moto, na wataalamu wa uhandisi wa kijeshi.
2.
Jeshi la Anga (Air Force):
- Huhusika na ulinzi wa anga la nchi, upelelezi wa angani, na mashambulizi ya angani inapohitajika.
- Vinasimamia ndege za kivita, helikopta, mifumo ya makombora ya ulinzi wa anga, na teknolojia za rada.
3.
Jeshi la Majini (Navy):
- Huhusika na ulinzi wa mipaka ya maji (bahari, maziwa, au mito) na kuhakikisha usalama wa njia za maji.
- Vinasimamia meli za kivita, manowari, boti za doria, na vikosi vya majini (marines) kwa operesheni za pwani.
- Muundo huu ni muhimu hasa kwa nchi zilizo na pwani au visiwa.
4.
Vikosi vya Ziada au Maalum:
-
Vikosi vya Operesheni Maalum (Special Forces): Hawa ni askari waliofunzwa kwa ajili ya misheni za siri, za hatari kubwa, au za kiufundi kama uokoaji, upelelezi wa kina, au vita vya msituni.
-
Vikosi vya Upelelezi (Intelligence Units): Huhusika na kukusanya taarifa za kijeshi na za usalama.
-
Vikosi vya Usaidizi (Logistics and Support): Huhakikisha usambazaji wa chakula, vifaa, silaha, na huduma za matibabu kwa askari.
- *
Vikosi vya Teknolojia na Cybersecurity *: Katika enzi ya kisasa, jeshi linahitaji wataalamu wa vita vya saiberneti ili kulinda miundombinu ya kidijitali dhidi ya mashambulizi ya mtandao.
Vikosi hivi vyote kila kimoja kina kazi yake ya kufanya kwa pamoja kushirikiana na vikosi vingine katika Operation zao kila mmoja anafanya kwa nafasi yake, Mfano Israel walipoigaragaza Iran kuanzia June 13-24,2025 vikosi vilivyoshiriki ni vingi kila kimoja kwa nafasi yake kwa hiyo nakushangaa unaposema na kusifia sana Jeshi la anga la Israel(IAF) na ukawapuuza Askari wa miguu wa Israel huko ni kuonyesha umbumbumbu wako katika mambo ya kijeshi.
Kwanza inabidi ujue kuwa katika Majeshi yote wa mhimu sana ni askari wa miguu (Infantry) wala si Ndege-Vita( Air-Force) kama mnavyowapamba kwa sababu Kijeshi Ndege na Mizinga ni silaha za misaada tu( Support weapons)
Mfano mzuri Ndege-Vita za Israel ni kweli ziliweza kulidhibiti anga lote la Iran kwa siku 12 hawakuweza kurusha hata ndege-Vita zao kuhofia kudunguliwa au kupambana na ndege-Vita za Israel. Na pia waliweza kwenda na kupiga popote Iran bila kuzuiwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran ambayo kwa wakati huo ilikuwa haifanyi kazi nasema ilikuwa haifanyi kazi kwa sababu kwa kipindi cha siku 12 hatukuona wakifurukuta mbele ya wanahewa wa Israel.Baada ya mkataba wa Amani Iran kukubali ndege-Vita za Israel zilitoka huko na ndiyo ukawa mwisho wa udhibiti wa Israel kwenye anga la Iran.
Mfano mzuri wa Pili Hezbollah baada ya Oct 07,2023 walianza kurusha vikombola vyao huko kaskazini mwa Israe hatimaye iliamua kula sahani moja na magaidi hao baada ya Operation Beeper 📟 na kuuwawa Gaidi Hassan Nasrallah Hezbollah walitepeta hivyo kuamua kusaini mkataba wa Amani wakati huo askari wa miguu wa Israel tayari walikuwa wako ndani kabisa mwa Lebanon ng’ambo ya mto Litan kumewafanya mpaka leo hii askari hao wawepo huko kusini mwa Lebanon.
Kwa hiyo bila shaka yoyote umeona tofauti ya operation mbili hizo na ipi ya mhimu katika jeshi lolote. Nakushauri tu usipende kufakamia field za watu kwa ujuaji wa namna kitu!!!