Kheri ungeuliza uelezewe umeandika utumbo mtupu.
IDF ni jeshi ambalo halina ufanisi wowote.
IDF vita za cross fire hawawezi ndiomaana wanaua raia hovyo.
Hamas haijifichi nyuma ya raia na wanavaa sare zao kama za jeshi.
Israel inafanya genocide ndio maana mwaka Jana waliua mateka wao wenyewe wanne,mateka walivua mashati na kuyapeperusha wakitaka kuokolewa video footages zilionesha askari watatu wa IDF wakiwamiminia risasi. Kusogea karibu ndio wanagundua wameua raia wao wenyewe.
Sio tu Gaza tuje Lebanon, Hizbollah ilipoanza kuirudishia Israel mashambulizi Israel kuona inazidiwa ikawa inalipua Central Lebanon ilhali vita ipo South Lebanon. Kwa akili zako hivi inaingia akili maadui wapo Namanga wewe unalipua Tanga!?
Israel inaua raia kimakusudi ili kuwatia hofu wapiganaji wajisalimishe.
Hiyo mbinu waliitumia Lebanon ikawalazimu Hizbollah kusalimu amri.
Majeshi yenye ufanisi ni kama vile jeshi la Uturuki.
Mwaka huu huu mwanzoni jeshi la Uturuki lilipeleka infantry 160 tu kukabiliana na waasi wa Kurdish.
Tena hao wanajeshi walienda na armoured vehicles tu hawakuenda na ndege wala nini.
Na hakuna raia wa Syria aliyeumizwa hata mmoja. Na Kurdish fighters huwa wanavaa kiraia. Ila walitandikwa balaa .
We unataja IDF?
Halafu pia umetudanganya hapo kusema eti Israel ilitawala anga la Iran kwa wiki nzima,embu wacha uongo.
Israel ilikua ikishambulia kwa kushtukiza na kupumzika tena hususan pale ADS za Iran bavaar-373 ziliporudishwa kazini.
Israel hakuwahi kumiliki anga la Iran.
Kama angemiliki anga la Iran kwa mashambulizi ya ndege 150+ leo hii Iran ingekua kote magofu.
Kama hamujui ulizeni msijiandikie mahisia yenu humu yasiyo na kichwa wala akili.