Hivi kuna madhara gani kwa Mtu pale anapojizuia kutoa/kuachia gesi kwa muda mrefu?

Hivi kuna madhara gani kwa Mtu pale anapojizuia kutoa/kuachia gesi kwa muda mrefu?

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
5,882
Reaction score
5,087
Iwe kwa makusudi tu au kwa sababu ya mazingira magumu yanayomzunguka Mtu.

Wapo wale ambao shughuli zao za kila siku hujumuisha kuzungukwa na Mtu au watu wengine,na isivyo bahati kitendo hiki cha kuruhusu gesi kutoka ni tendo linalosababisha fadhaa kubwa kwa Muhusika pale anaposikika na Mtu au Watu wenzake.

Na pale inapokuwa uliokuwa nao/naye ni Mgeni ndio hali huwa ngumu zaidii.Hapa ndio pale Mtu kama Dereva wa Mtu/Watu,Wafanyakazi wa ofisini nk kutamani wangekuwa bodaboda au Fundi Wajenzi n.k. wenye uhuru wa kujiachia watakavyo.
 
Ukitaka kujua madhara yake fululiza kula haragwe na michips alafu jaribu kubana kwa wiki nzima utapata majibu
Kula mboga mboga matunda na maji kwa wingi kuepuka hiyo fedheha hataikitokea umepumua hakinuki🤣🤣
 
Aina hii ya vijana wana mchango mdogo sana kwa Taifa
Kwanza mimi sio kijana,pili ina maana wewe huoni hoja hapo?.

Mimi nimehoji athari za kiafya iwapo Mtu snajizuia siku nzima ili hali "gesimwili' inabisha hodi kila muda na Mtu huyo kuona ni sawa tu.

Nahitaji ushauri wa kitaalamu ikiwezekana Watu wsshauriwe cha kufany au la kama haina tatizo pia tujue,ndio maana linaitwa jukwaa la afya.
 
wataalam wa afya wanashauri kuwa ni vyema mtu ajisikie huru kupitisha gesi pale inapobidi kwa staha na mazingira yanayofaa.
 
Ndio maana hapo nikataja baadhi ya kada ambazo hawana kikwazo,mfano Machinga,bodaboda,Fundi ujenzi nk.,tofauti na yule ambaye shughuli zake zinamuweka katikati ya Watu au Mtu mwingine muda wote,bila shaka huyo madhara yatamkuta.
wataalam wa afya wanashauri kuwa ni vyema mtu ajisikie huru kupitisha gesi pale inapobidi kwa staha na mazingira yanayofaa.
 
Ebu fikiria mtu kama Samia au Philip mpango au majaliwa muda wote wana watu wamewazunguka,watu kama hao wakitaka kujamba inakuaje?
 
Back
Top Bottom