Tulikua kijiweni tunapoteza muda,jamaa mmoja akatuambia anataka ajilipue aende India kutafuta maisha.
Nikawaza,then nikaingia youtube kucheck maisha ya wahindi wenyewe tu huko India ni mara mia ya hapa kwetu.
Hivi kuna mtanzania aliwahi kwenda kujitafuta India akatoboa?
Nina hoja fikirishi japo nadhani sitakuwa nimetoka nje ya mada!
Umesema maisha ya wahindi huko India ni mara mia ya hapa kwetu!
Lakini India ina viwanda vikubwa vinavyotengeneza bidhaa ambazo zina soko kubwa hapa Tanzania.
Moja ya bidhaa zilizotengenezwa India zenye soko hapa TZ ni mabasi na malori aina ya TATA na EICHIER.
Pia kuna pikipiki aina ya BOXER , TVS na HERO.
Pia BAJAJI aina zote zilizopo hapa TZ zote ni ,made in INDIA.
Pharmacy zetu zimejaa madawa ya aina mbalimbali ambayo yameandikwa MADE IN INDIA.
Lakini India imekuwa na hospitali zenye madaktari bingwa hospitali ambazo zimekuwa kimbilio la watanzania wengi wenye vipato vinavyowaruhusu kufika huko kutibiwa maradhi mbalimbali sugu hasa magonjwa ya moyo, sukari na figo.
Zaidi ya hayo India ina wasanii wa wa filamu ambao wanapendwa sana na sehemu kubwa ya watanzania kuanzia akina Amita bachan ,Dharmendra, Mithun Chakraborty, Shaturghan Sinha hadi akina Shah rukh khan,Ajay Devgan,Sunil Shetty nk.
Pia kuna wasanii wa kike kama akina Karisma Kapoor, Ravena Tandom, Juhi Chawla na wengine ambao nimewaacha kuwataja ili kuokoa muda.
Swali ni kwamba SISI WATANZANIA TUNA BIDHAA GANI TULIYOTENGENEZA AMBAYO TUNAWEZA KUUZA INDIA?!
JE BIDHAA ZETU ZA KILIMO KAMA MAEMBE , PARACHICHI NA NDIZI YANA NAFASI YA KUPATA SOKO HUKO INDIA?
Swala la watanzania kutokupata fursa ya maisha huko India ni kutokana mfumo wa siasa za kiuchumi za India.
India ni nchi Tajiri yenye mfumo wa kibepari!
India ina matajiri wakubwa wenye utajiri uliopindukia ambao ni wachache halafu inao masikini wengi sana wenye umasikini uliopindukia.
Siyo rahisi mtu mweusi kwenda kutafuta maisha India akatoboa kwa sababu pamoja na kwamba India ni moja ya nchi zilizoendelea kiuchumi na kijeshi (India ni moja ya nchi chache zinazomiliki nyuklia ) bado nchi hiyo inao masikini wengi ambao ni walala hoi kama sisi.
Sasa mgeni hawezi toboa katika nchi ambayo bado kuna wenyeji wengisana wanaojitafuta lakini bado nasema masikini wa India kiakili yuko na afadhali sana kuliko masikini wa Tanzania na ndio maana masikini wa India akipata nafasi ya kutoroka nchi yake na kuingia Tanzania ndani ya miaka michache anageuka kuwa milionea na baadae bilionea wakati watanzania wakiendelea kuogelea ndani ya umasikini ndani ya nchi yao.