Hivi kuna mtanzania amewahi kwenda kutafuta maisha nchini India akatoboa?

Hivi kuna mtanzania amewahi kwenda kutafuta maisha nchini India akatoboa?

watanzania wengi naowasikia leo kuwa wapo nchi za Ulaya na Asia kuanzia miaka ya Mwanzoni ya 70, maka ya 60 na Kabla, elewa kuwa safari yao ilianzia bandari ya Dar kuelekea India.

Enzi hizo usafiri pekee wa rahisi na urahisi wa kuchomoka Tanzania / Tanganyika ulikuwa kupitia Inda kwa meli mbili marufu ziizokuwa zikija Dar, nazo n MV Karanja na MV Haryana.

Mabaharia walioelekea Ugiriki enzi hizo hiyo ndiyo ilikuwa route yao kuu.

Licha ya hayo. India na Bandari za Tanzania zina maingiliano na uhusiano mkubwa Kihistoria wa kibiashara kabla sana ya ujio wa wakoloni wa kizungu.

una kabila la Kiafrika India na Pakistan ambalo kwa asilimia kubwa asili yao ni Afrika Mashariki.

Bila kutafuna maneno, kumbuka kuwa una wajomba na shangazi zako huko Kihistoria kuna mpaka tawala za Kiafrika, India.

Kuna sehemu nilisoma namna hao weusi wanateseka huko na kutamani hata warudi Afrika, yaani weusi huteseka sana kwenye hayo manchi yakiwemo uarabuni.
 
Hizi thamani za hela mbona zinawapumbaza wengi sana.
Yen ya Japan inalingana na Shilingi ya Kenya, kwa hiyo Kenya inalingana na Japan?
Pound moja ya Uingereza ni sawa na yuan 10 za kichina,
Hujaelewa context ya swali lake na alilenga wapi na watu wa aina gani!

Vijana wzamiaji, Kijana akizamia India ukafanya "vibarua" vya India huwezi kutoboa kwa vile ni masikini na hela yao haina nguvu ukiipata ukaibadili kwa dola ya kuja nayo unapata dola kidogo.

USA ukibahatika kufanya vibarua, kwa thamani ya dola against Tsh, ukirudi unakuwa na kitu! Nadhani alilenga kwenye vitu kama hivyo. Nguvu ya hela ya nchi uliyopo and how much are you earning!

Nikupe mfano wa experience ya kijana wetu kazini those days : aliishi Thailand 30 yrs back. alikuwa sponsored na Switzerland gov. alikuwa analipwa in US dola. according to him, alikuwa anatumia dola 100 kila kitu, pango, nauli, chakula etc etc maana ukibadilisha hela ya baht unapata nyingi kwa dola 100 ya kuishi mwezi mzima , then you save a lot!....... stipend yake was around USD 700 per month! alikaa miaka 3...alirudi na gari mbili, akajenga nyumba akahamia na kununua shamba Kibaha na kufuga................those days.
 
Listen my brother ,money is everywhere in the world
Wherever you go people are sick of life hacks ,they suffer so how do you help them? They have bucks to find solutions

Unaenda india kufanya nn ? Huwezi sema kazi yoyote ,amna kazi yoyote kama una ujuzi wa computer yan wew ni mkali wa programming india issa baby ukienda hukosi kazi.

Kabla hujasafiri lazima ujifunze kazi nyingi ujuzi ndio nguzo.

Huku Tanzanian mnasema kuna maisha magumu lakin watu toka njee wanakuja na wana pata maisha .

Kuna watu hapa Tanzanian wanalipwa hadi million 50 nakuendelea kwa mwenzi na sio wafanya biashara ni professionals tu lakin ujuzi wao sio mchezo


Kwaio kama huna ujuzi hata ulaya usiende sikuiz matumizi ya nguvu yamepungua
 
Sijawahi kusikia nilokwenda kule kikazi mwaka jana sasa kwenye hoteli niliyofikia mlinzi wa pale hotelini akaniomba nimfanyie mpango wa yeye kuja Tanzania kufanya kazi ya Ulinzi, nilimjibu haiwezekani.
Nikamuuliza mshahara wake nakumbuka ilikuwa kama rupee elfu 80 kama laki 2 na nusu ya kibongo nikamjibu huku Tz mshahara ni kama huo ila kwa mhindi hawezi kukubaliwa kuwa mlinzi Tanzania labda kwa professionals.
Jamaa alisikitika sana kwa mimi kukataa kumsaidia kuja bongo kuwa mlinzi.
Kule maisha ni magumu sana kule kuna maskini huku bongo hakuna maskini kama wale .
Kule kuna watu ukoo mzima haumiliki hata kijipande cha ardhi hata vijijini.
Huku bongo unakutana na maskini ila ana miliki ardhi huko kijijini kwao ,kule hakuna .
Kuna siku nilitembelea ubalozini nikakutana na dada wa kibongo analia kwamba alidanganywa kuna kazi akapelekwa kule akaishia kwenye danguro akawa anafanyishwa kazi za sex halipwi chochote zaidi ya kupewa msosi.
Siku hiyo alibahatika kutoroka akakimbilia ubalozini passport hana walikuwa wamemnyang'anya ubalozi ndio ukawa unawasiliana napolisi waende kuchukua passport yake.
Kali kulipo yote hapo ubalozini siku hiyo nikakutana na mhindi mbongo .
Huyo mhindi mbongo alikwenda India kusalimia bibi yake alikuwa mgonjwa sasa akakaa hadi passport yake ya kibongo ikaexpire sasa akawa anataka atengenezewe passport nyingine na ile fomu kuna sehemu inatakiwa ijazwe na mdhamini ambaye lazima awe mbongo akawa ananiomba nimjazie nikawauliza wale maofisa wa ubalozini kwa nini wasimjazie wao wakanijibu wao hawaruhusiwi. Wale maofisa waliniomba sana nimsaidie eti ni mtanzania mwezangu nilimjazia kwa shingo uoande sana manake ninavyowachukia wahindi basi tu.
Ila jamaa alikuwa anaongea kiswahili fresh aliniambia anaishi mitaa ya kariakoo.
Jamaa anakwambia mishe zake zote ni bongo kule hapafai.
India asikwambie mtu ni nchi moja ya hovyo sana ila wanaigeria noma wale jamaa niliwakuta kule hadi wana maduka na vimgahawa wanakomaa na wahindi .
Siwezi kamwe kumshauri mtu aende India kutafuta maisha
Yo have spoken the truth i have a friend, ni muhindi ame graduate medical aise the guy used to show videos of schools amepita hata vyoo hamna he says ni poorest village yeye ni youtuber ,gamer kwa sasa huku akikimbiza kaz ya professional yake

India ni maskini japo ni kuna upande ni matajir sana.

Wafrica wengi wanaend Singapore hasa wanunuzi wa magari
 
Tulikua kijiweni tunapoteza muda,jamaa mmoja akatuambia anataka ajilipue aende India kutafuta maisha.
Nikawaza,then nikaingia youtube kucheck maisha ya wahindi wenyewe tu huko India ni mara mia ya hapa kwetu.
Hivi kuna mtanzania aliwahi kwenda kujitafuta India akatoboa?
Wahindi tu ambao ni homeless (wanaoishi mitaani na familia zao) wako zaidi ya 30 Million. Maisha ni magumu kuna tabaka linaitwa "untouchables" halina mali. Sasa wewe utoke uende India kutafuta maisha, HUTOBOI kamwe.
 
SURE!!!!!!! Rafiki yangu mmoja alikuwa anafanya kazi hospitali moja ya mhindi hapa Tanzania. Alimpiga dola 40,000/-akajenga nyumba nzuri baada ya mwezi ilinyumba iliuungua yote.
Mimi niliwahi kumpiga muhindi kipindo nipo kija mdigo ata miaka 30 sijafika sasa mambo ya ujana nikanunua Falat screen , Fridge, Home theater na nikawa nafanya biashara ya mbao kutoka Tabora, Sasa kimbembe kikaanza TV ikapasuka Fridge likaharibika, TV mpaka leo ipo kwa fundi na Fridge nililitengeneza nikaliuza kwa rafiki yanu na yeye likamfia akaliacha kwa fundi, Biashara yangu ya milango ya mbao ikafa treni ilipinduka. Najuta bora ningenunua ardhi kigamboni sasa hivi ningekua tajiri. Mwenzagu yeye tulie piga nae pesa yeye aliniamba alinunua kiwanja Kisalawe na amejenga nyumba imeishia kwenye linta lakini naamini kashauza maana wahindi siyo watu wazuri, ningekua nimepiga mzungu naamini ningekua mbali.
 
Kwanini mtu akienda Ulaya au Amerika hata kwa mwaka mmoja akirudi anakuwa kabadili lafudhi ila akienda India hata miaka 30 anarudi na lafudhi yake ileile?
Mkuu wahindi hawataki lugha yao jamii nyingi waijue kwa kusoma ata kwa kujifuta tu sehemu ya kazi au Nyumbani tofauti na nchi zingine, Wewe unaweza ukafanya kazi kwa wahindi ata miaka 10 na lugha yao usiifaham na mimi nikafanya kazi na Mwarabu miaka 3 nikajua lugha yao.
 
Ila wahindi wanapamba aisee jamaa wanapiga kazi wale kama wendawazimu ukiwaona asubuhi wanavyokwenda makazini na jioni wanavyorudi walivyojazana kwenye matreni yao ya bei rahisi unaweza hisi ni wendawazimu wengine wanakaa hadi juu ya treni utafikiri hawalipi nauli
Mkuu ile ni kweli wanakaa juu ya treni au Maigizo ya filamu?
 
Tushakaa sana umangani, Pakistan, Afghanistan na Iran, wapo wengi waliotoboa na wapo wengi walioshia kula bata na wapo walioshindwa kabisa kutoboa.

Kutoboa au kutotoboa wakati mwingine ni wewe mwenyewe, juhudi zako, bahati yako, namna unavyoishi na unyenyekevu wako mbele za Mwenyezi Mungu.

uelekeo Fallujah - Iraq.
 
Back
Top Bottom