Hivi kuna mtanzania amewahi kwenda kutafuta maisha nchini India akatoboa?

Haaahaa πŸ˜† 🀣 kwaio kafara haisaidii
 
Hao ni hatare Sana Sanaa mkuu kweli tembea ujionee
 
Asilimia 80 huyo sio Muhindi as in India bali ni Mpakistan; 79.8 percent ya Wahindi ni Hindus na ulichoweka hapo ni Arabic ambayo ipo kwenye Quran; Indeed, we belong to Allah and to Him we will return.
True,
ndio JAMII hizo izo za wa Pakistani.
 
Maisha mzee hayapo hivyo,ukiwa na mindset hiyo hutoboi..Kuna watu wametoka Mgeta morogoro wamekuja Dar wametoboa,na Kuna waliotoka dar wameenda Mgeta wakalima njegere wakatoboa,..kufanikiwa sio mahali,ni kuona fursa and to take advantage of it,

Kuna girl miaka mitano nyuma alikua India anasoma Aviation,alikua anafanya hustle ya kutafuta wanafunzi wakitanzania wakasome katika college aliyo kuwepo chuo kinampa commission,.chuo kamaliza now ana hela anaishi India kazi yake Kama "middleman" ukitaka kitu toka India,au muhindi akitaka kitu toka Tanzania
 
India ni another shithole, a bigger one in that case. Ukienda huko utarudi masikini mara 5 ya mwanzo.
 
Ila africa kuna tatizo sana,kabisa mtu unasema mlikua kijiweni mnapoteza muda?
Huo muda mliopoteza mtaufidiaje?
Tupo duniani kuishi siyo kupigania maisha...

Mabepari yametu-brainwash kuwa hututakiwi kukaa kijiweni,,, ila tuwe maroboti ya kuwatengenezea hela za kodi na kununua bidhaa zao..
 
Hata masweta ya shule yanapatikana India kwa bei nafuu kuliko China.
 
huwezi kutoboa ambako thamani ya hela yako na huko uliko India hazina tofauti kubwa
Indian Rupee 1 = 31.2261 Tanzanian Shilling

while US Dollar 1 = 2,681.47 Tanzanian Shilling........................... huku naweza kutoboa
umejielekeza vbaya hiko sio kigezo pekee cha utoboaji
 
Nina hoja fikirishi japo nadhani sitakuwa nimetoka nje ya mada!
Umesema maisha ya wahindi huko India ni mara mia ya hapa kwetu!
Lakini India ina viwanda vikubwa vinavyotengeneza bidhaa ambazo zina soko kubwa hapa Tanzania.
Moja ya bidhaa zilizotengenezwa India zenye soko hapa TZ ni mabasi na malori aina ya TATA na EICHIER.
Pia kuna pikipiki aina ya BOXER , TVS na HERO.
Pia BAJAJI aina zote zilizopo hapa TZ zote ni ,made in INDIA.
Pharmacy zetu zimejaa madawa ya aina mbalimbali ambayo yameandikwa MADE IN INDIA.
Lakini India imekuwa na hospitali zenye madaktari bingwa hospitali ambazo zimekuwa kimbilio la watanzania wengi wenye vipato vinavyowaruhusu kufika huko kutibiwa maradhi mbalimbali sugu hasa magonjwa ya moyo, sukari na figo.
Zaidi ya hayo India ina wasanii wa wa filamu ambao wanapendwa sana na sehemu kubwa ya watanzania kuanzia akina Amita bachan ,Dharmendra, Mithun Chakraborty, Shaturghan Sinha hadi akina Shah rukh khan,Ajay Devgan,Sunil Shetty nk.
Pia kuna wasanii wa kike kama akina Karisma Kapoor, Ravena Tandom, Juhi Chawla na wengine ambao nimewaacha kuwataja ili kuokoa muda.
Swali ni kwamba SISI WATANZANIA TUNA BIDHAA GANI TULIYOTENGENEZA AMBAYO TUNAWEZA KUUZA INDIA?!
JE BIDHAA ZETU ZA KILIMO KAMA MAEMBE , PARACHICHI NA NDIZI YANA NAFASI YA KUPATA SOKO HUKO INDIA?
Swala la watanzania kutokupata fursa ya maisha huko India ni kutokana mfumo wa siasa za kiuchumi za India.
India ni nchi Tajiri yenye mfumo wa kibepari!
India ina matajiri wakubwa wenye utajiri uliopindukia ambao ni wachache halafu inao masikini wengi sana wenye umasikini uliopindukia.
Siyo rahisi mtu mweusi kwenda kutafuta maisha India akatoboa kwa sababu pamoja na kwamba India ni moja ya nchi zilizoendelea kiuchumi na kijeshi (India ni moja ya nchi chache zinazomiliki nyuklia ) bado nchi hiyo inao masikini wengi ambao ni walala hoi kama sisi.
Sasa mgeni hawezi toboa katika nchi ambayo bado kuna wenyeji wengisana wanaojitafuta lakini bado nasema masikini wa India kiakili yuko na afadhali sana kuliko masikini wa Tanzania na ndio maana masikini wa India akipata nafasi ya kutoroka nchi yake na kuingia Tanzania ndani ya miaka michache anageuka kuwa milionea na baadae bilionea wakati watanzania wakiendelea kuogelea ndani ya umasikini ndani ya nchi yao.
 
Inchi yeyote duniani unaweza pata pesa au ikawa ngumu kwako kutoboa ,
. inategemea mwenyeji wako aliyekupokea ana michongo gani?

Elewa neno mwenyeji wako ana michongo gani??

Hata hapo Tanzania unapoona pagumu ,, ukipewa mchongo wa pesa hata ulaya au Canada utaona unapoteza muda.
 
huwezi kutoboa ambako thamani ya hela yako na huko uliko India hazina tofauti kubwa
Indian Rupee 1 = 31.2261 Tanzanian Shilling

while US Dollar 1 = 2,681.47 Tanzanian Shilling........................... huku naweza kutoboa
Hizi thamani za hela mbona zinawapumbaza wengi sana.
Yen ya Japan inalingana na Shilingi ya Kenya, kwa hiyo Kenya inalingana na Japan?
Pound moja ya Uingereza ni sawa na yuan 10 za kichina,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…