Umeandika kama vile sijaelewa kabisa kama kuna hasara inapatikana, anyway tayaache hayo. Kweli hii ni mada pana sana na ndio maana hata ule mfano wako wa Fastjet haukuwa sahihi kwani ile ni airline ambayo ni LCC. Na pia inatoka nje ya nchi na ni rahisi kwao ku-target kaeneo/ route moja yenye faida bila kujali mengine.
Nisikuchoshe sana, msingi wa hoja yangu ni hivi, solution sio kutowekeza kwenye airline business na kuwanyima watu huduma hiyo kabisa, bali kuangalia maeneo ambayo ni vyanzo vya hasara ya biashara. Nilitaja machache, aina za ndege ziendane na operations husika/( mfano huwezi kupata hasara kwa kwenda Iringa kwa kutumia Bombardier Q 300) au kuangali suala la kuwa na Dreamliner kama haina route, gharama na maintenance kwa kuwekeza kuwa na wataalamu wa ndani na effective management kwa ujumla. Hivi vyote viwe kwenye mpango wa biashara.
Lengo iwe pia kutumia Airline kuwezesha sector nyingine za kiuchumi, i.e tourism. Fastjet hawawezi kuwa na malengo kama hayo.
Mwisho wa siku kila anayefanya biashara hii anajua ni biashara yenye faida ndogo ( small marginal profit).
Hatahivyo, mbona wenzetu wanawekeza kwenye hicho kilimo na wana ndege?!?