Hivi kuna ndege imeshatua Chato tangu baada ya mazishi?

Halafu watu walikuwa wanasema jamaa ana maono.
Nakumbuka kipindi Msuya Ni waziri mkuu, mji wa Mwanga ulipewa upendeleo wa hali ya juu. Mwanga kulikua na simu za STD wakati Sumbawanga na Songea ambayo Ni miji ya mikoa kulikua hakuna hiyo huduma (kwa wanangu simu ya STD Ni Ile ambayo unapiga moja kwa moja bila kumuomba operator )
Jengo la NSSF Mwanga lilikua Ni zaidi ya majengo ya mikoa. Lakini Kiko wapi. Mwanga mpaka saa hii Ni Kijiji tu hata stendi hakina.
 
Kumbe tuna case study nzuri kabisa! Hata Hedaru kwetu ninaona inasonga mbele Zaidi ya Mwanga!
 
Ipo ndege pale ya kunyunyiza viwatilifu inasubiri uvamizi wa makundi ya nzige
 
Unataka ndege itue kufanya nini sasa hayo majungu kiongozi
 
Hilo liuwanja Lina faida gani kwa nchi na watu wa chato? Acha mawazo mgando kwani ungekuwa mwanza Nani angepinga?
Mbona mimi nipo kwenye wilaya ina uwanja wa ndege na inatua siku moja moja kuleta madawa ya hospitali, mbona hamlalamiki punguzeni unafiki na utundulisu wa kupinga kupinga kila kitu
 
Well, kama kuna bombardier inaenda Dodoma na inaenda Songwe why isichukue na abiria 24 wa Iringa🤷
 
Mbona mimi nipo kwenye wilaya ina uwanja wa ndege na inatua siku moja moja kuleta madawa ya hospital mbona hamlalamiki punguzeni unafiki na utundulisu wa kupinga kupinga kila kitu
Huo uwanja wa Wilayani kwenu una ukubwa gani? Umejengwa kwa gharama ya sh ngapi? Ukilinganishwa na wa Chato ambayo tangu ipewe wilaya hata miaka 10 bado. Mkuu uwe unajielewa siyo kuunga mkoni kila kitu hata kwenye mambo ya kijinga yanayoligharimu Taifa.

Ebu angalia ule uwanja umejengwa gizani, bunge halijui gharama zilizotumika na utaratibu wa kumpata mkandarasi na liuwanja lenyewe runway yake sawa na wa DSM
 
Air Tanzania inakwenda mara tatu kwa wiki. Leo Jumatatu ndege 5H TCD imekwenda kama flight TC 131 ikielekea Mwanza kupitia Chato na saa saba mchana ilikuwa imetua.
 
Well, kama kuna bombardier inaenda Dodoma na inaenda songwe why isichukue na abiria 24 wa iringa🤷
Hiyo fuel cost na landing charges za Dodoma -Iringa bado mathematics don't add up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…