Ni ngumu kuacha ila unaweza fanya jambo ambalo litakufanya usijisikie vibaya unapobet na kupoteza.
Mfano, unaweza kujiwekea kuwa kabla hujabeti pesa yoyote, 50% ya hiyo pesa unamtumia mzazi, au unanunua kitu muhimu au una lipa kadeni fulani, au unaweka sehemu ambayo huwezi ifikia.
Fanya hivyo kwa miezi kadhaa huku ukiendelea kuiongeza hiyo 50% mpaka ifike 70%. Ikifika 70% we endelea kubet hiyo 30% utashangaa tu kuna siku utaona ni ujinga utaacha na hata usipoacha hutajisikia kuwa umepoteza 100% na ile 70% itakuwa imefanya kitu, ikitokea umeshinda jitahidi 100% ya ushindi inaenda ilipoenda 70% sio 30%.
NB: Zile bet unazoshinda jitahidi usibet, fanya kitu kingine kabisa na ukiona unashindwa basi fata mwongozo ule ule wa 70% 30%.