Hivi kuna njia yoyote ya kuacha kubet?

Hivi kuna njia yoyote ya kuacha kubet?

Ukitaka kuacha kubeti chagua Ile timu unayoiamini kabisa ikicheza na timu kibonde kabisa ipe win or draw then tupia kamilioni, kakiliwa utaacha milele kubeti. Kama sijasahau 2017/2018 msimu ambao Barcelona anaongoza ligi kashinda mechi 15 mfululizo bado mechi tatu wamalize msimu na alikuwa hajafungwa hata mechi moja. So ni kama ilivyo liverkusen sasa hivi, ni kaamini anaisaka rekodi ya arsenal kumaliza ligi bila kufungwa. Basi bhana mechi ya 36 Barcelona anakutana na Levante, tena akiwa nyumbani, nikampa Barcelona win or draw then nikatupia laki sita. Full time Levante 5 Barcelona 4. Mpaka Leo betting naiona kama gereza Wala sio kituo Cha polisi
 
kubeti ni tamaa ya kutoa kidogo na kupata kingi ndani ya muda mchache imetufanya vijana wengi tuishi kwenye dibwi la kubahatisha na kutaka vya haraka mpaka wengi wetu hudondokea kwenye madhara ya ushoga na liwati.

Jamii inaharibika kwa kuwa betting inadhoofisha akili na vijana wengi hatufanyi planning na kuanalyse mipango ya uchumi ili kuleta tija kwenye taifa hatimae tunadondokea kwenye ulevi mbaya kupindukia.

Ni zipi njia sahihi za kuacha kamari?
Hata pombe inaharibu vijana kwenye jamii, lakini haijaacha kunywewa na watu wenye busara!
 
Wanasemaga odds chache unatia mzigo hapo uhakika😎😎..sasa kama wewe ulikua unebet mechi55 utalia sana nenda kule wazee wa mkeka waombe ushauli upya.
 
Hakuna tabia ambayo mwanadamu huwezi kuiacha ikiwa utaamua kwa dhati kabisa kutoka moyoni.

Uraibu wowote unaweza kuuacha ikiwa utaweka mkakati. Futa apps zote za mpira kwenye simu yako, futa apps zote za kubeti kwenye simu yako wala usifuatulie jambo linalohusiana na kubeti kwa muda wa mwezi mmoja na siku kumi. Hakika utaacha kubeti kirahisi tu.

Jiweke busy na shughuli za maendeleo.
 
Ukiona hivi ujue unakaribia kuacha.
Kwanza kabisa ujue Betting ni njia ya kuutafuta umasikini kwa nguvu nyingi.
Kaa soba ikiwezekaba nenda kajitenge kwa miezi kazaa vijiji vya mbali huko bila kutumia simu.
Sishauri hii njia rahisi ya kuikataa betting kwa dhati ni kuwa na simu lakini hufatili masuala ya kubeti.

Ukijitenga na simu itafikia kipindi utakuwa na kiu kali ya kubeti na ukiishika tu simu itakupelekea urudi tena kwenye betting kwa nguvu kali sana
 
Back
Top Bottom