Ukitaka kuacha kubeti chagua Ile timu unayoiamini kabisa ikicheza na timu kibonde kabisa ipe win or draw then tupia kamilioni, kakiliwa utaacha milele kubeti. Kama sijasahau 2017/2018 msimu ambao Barcelona anaongoza ligi kashinda mechi 15 mfululizo bado mechi tatu wamalize msimu na alikuwa hajafungwa hata mechi moja. So ni kama ilivyo liverkusen sasa hivi, ni kaamini anaisaka rekodi ya arsenal kumaliza ligi bila kufungwa. Basi bhana mechi ya 36 Barcelona anakutana na Levante, tena akiwa nyumbani, nikampa Barcelona win or draw then nikatupia laki sita. Full time Levante 5 Barcelona 4. Mpaka Leo betting naiona kama gereza Wala sio kituo Cha polisi