Hapo nyinyi mnashindwa kuelewana ndio maana kila mtu atavutia upande wake.
Hapo mimi nilichoelewa ni kwamba;
Kwa upande wa uislam;
Hapo wanaongelewa wale wanawake waislamu ambao wanaishi kwa kufuata misingi na sheria ya dini yao ya kiislamu (waumini), na sio wanawake wale wanaoitwa waislamu kwa majina tu.
Kwa upande wa ukristo;
Hapo pia wanaongelewa wanawake wakristo wale wanaofuata misingi ya dini ya kikristo na sheria zake.(waumini)
Sasa makundi yote mawili haya ukiwaweka pamoja katika mazingira wezeshi yaani maji sio shida, pesa ipo na muda pia upo utaona utofauti wao katika suala zima la usafi.
Mimi nitatoa shuhuda kwa nilichoona kwa macho yangu.
Kwenda haja
Huwezi kumkuta bint (muumin) wa kiislam akienda msalani bila maji, haijalishi ni haja kubwa au ndogo. Kwa mafundisho ya dini ya kiislam kinyesi, na mkojo ni najisi.
Wanawake wa kikristo mara nyingi hutumia maji kwaajili ya haja kubwa tu, kama itatokea ametumia maji kwa haja ndogo basi atakuwa ana dharula nyingine lakini sio atumie maji kwasababu kaenda kukojoa, na (asilimia kubwa hawa ndio wanaambukiza U.T.I kwasababu ya kutojisafisha njia ya mkojo inapotumika)
Kuvaa Mawigi na Kufuga Rasta
Bint wa kiislam huwezi mkuta kafuga Rasta au kaweka Wigi kichwani hayo yote ni haramu kwa mujibu wa dini, tena huruhusiwi kuswali au kuingia msikitini kama umeweka hayo madudu kwenye kichwa chako.
Bint wa kikristo ni kawaida kusuka Rasta na kuweka Wigi hata ukienda makanisani utawakuta wamevaa.
Rasta na Wigi husababisha uchafu kichwani na nywele kutoa harufu mbaya.
Kucha za Bandia
Haramu kwa muislam kuweka makucha ya bandia, ila kwa upande wa pili sijajua na sina uhakika sana kama biblia imekataza kuweka makucha ya bandia.
Hivi kwamfano ukimaliza kujisaidia haja kubwa unajisafisha vipi? Au ndio mnatumia paper kama akina Smith kule magharibi ya mbali! Kucha bandia huficha uchafu
Usafi katika nyumba za ibada/sehemu yakufanyia ibada.
Sehemu ya kufanyia ibada kwa mkristo hata ukivaa viatu ambavyo umekanyagia kinyesi ni sawa na hata kuingia navyo kanisani ruksa achilia mbali mavazi.
Msikitini huwezi kumkuta mtu anaingia na viatu lazima avue, anawe (kutia udhu) ndio aingie msikitini. Hata nyumbani pia lazima avue viatu atie udhu (kunawa) atandike mswala (mkeka mdogo wa kuswalia) ndio afanye ibada.
Al Islam Nadhif